March 4, 2019


VITA kubwa kwa sasa ipo kwenye ushindani wa kiatu cha ufungaji bora ambapo mpaka sasa kila mchrezaji anaendelea kuwasha moto kwa kutupia mabao kila anapopata nafasi mpaka sasa ikiwa ni mzunguko wa pili.

Msimu uliopita Emanuel Okwi wa Simba aliibuka mbabe wa ufungaji alimaliza akiwa na mabao 20 ila kwa sasa ana mabao sabaakiwa nafasi ya tano sawa na Emmanuel MMvuyekure wa KMC.

Kubwa la maadui kwa upachikaji wa mabao ni mshambuliaji wa Mwadui FC, Salim Aiyee ambaye ametupia mabao 14.

Nafasi ya pili inashikiliwa na wababe wawili Heritier Makambo wa Yanga na Meddie Kagere wa Simba hawa wote wana mabao 12.

Nafasi ya tatu ipo mikononi mwa watu wawili pia, Hassan Dilunga wa Ruvu Shooting pamoja na Eliud Ambokile aliyekuwa Mbeya City na kwa sasa amesepa yupo nchini Afrika Kusini.

Nafasi ya nne inakamatwa na watu watatu ambao ni Dickson Ambudo wa Alliance, Lyanga wa Coastal Union na John Bocco wa Simba.

Mzunguko wa pili ambao kwa sasa ni lala salama kila timu inapambana kutafuta matokeo huku kila kocha akijaribu kubadili mbinu kila baada ya kumaliza mchezo ili kupata matokeo chanya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic