March 4, 2019


BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Mada Maugo, amesema kuwa hatambui ushindi aliopewa mpinzani wake Twaha Kiduku katika pambano ambalo lilifanyika usiku wa jana  mwaka huu mjini Morogoro Stand Kuu ya Msavu.

Maugo amesema kuwa mwamuzi hakumtendea haki kwani tayari alishashinda pambano hilo la raundi 10, lilikatishwa ghafla kitu ambacho kinamuumiza na anataka pambano liludiwe.

"Mpaka raundi ya nane nilikuwa naongoza, mwamuzi aliamua kusimamisha shindano akidai nimempiga mpinzani wangu sehemu zizisohusika, kwa mwenye ujuzi alipaswa anionye sasa kumpa ushindi mpinzani wangu sio sawa.

"Mwamuzi Pembe Ndava,amenipokonya ushindi wangu na kutoa ushindi wa mezani, nataka gemu irudiwe kwa kuwa kitaalaamu huruhusiwi kukata pambano, chama cha ngumi za kulipwa kinatakiwa kilitazame hili kwa ukaribu," amesema Maugo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic