March 4, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amewaambia klabu ya Simba hawana uwezo wa kumsajili mshambuliaji wa klabu ya AS Vita Club, Jaen Mark Makusu. Imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa Zahera amewaeleza Simba kuwa hawatakuwa na uwezo wa kumlipa mchezaji huyo kwani kiwango cha malipo yake wao hawajawahi kukifanya kwa mchezaji yoyote yule.

Ameeleza Makusu amekuwa akilipwa kiasi cha mshahara wa milioni 39 kwa mwezi wakati Simba inatajwa mchezaji anayelipwa fedha ya juu ni Emmanuel Okwi anayepokea milioni 12.

Kauli ya Zahera imekuja kufuatia uwepo wa tetesi kuwa Simba ipo kwenye harakati za kumsajili Makusu ambaye yupo na VIta inayoshuka dimbani Jumamosi ya wiki hii kucheza na Al Ahly kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imetajwa kutaka saini ya mchezaji huyo ambaye wanaamini atawasaidia zaidi kwenye michezo ya kimataifa na hata Ligi Kuu Bara haswa kuiboresha safu ya ushambuliaji.

5 COMMENTS:

  1. Basis amchukue yeye akamlipe!

    ReplyDelete
  2. Huyu Zahera vipi mlopokaji tu kama wewe maskini usifikiri wote maskini usiseme twafa sema nakufa.

    ReplyDelete
  3. Huyu Zahera si anajuwa kuwa simba haitegemei mchango wa bakuli kuwalipa mamilioni ya usajili na mishahara uwezo wa Mo unajulikana kote Africa anao uwezo hata wakununua vilanu na wachezaji wake na yeye inamhusu nini kuingilia na wala hakutumwa anaogopa pindi akiipatikana mchezaji huyo yanga haitokuwa salama na uchungu mwengine Kakolanya kujiunga na simba na hata Manji siku zake angeliweza kumnunuwa mchezaji huyo

    ReplyDelete
  4. TATIZO ZAHERA HASOMI UKURASA HUU ILI APEWE USHAURI WA BURE. YEYE NI KOCHA TUNAMUHESHIMU TENA NI KOCHA WA TIMU KUBWA YENYE HISTORIA AJIHESHIMU SIO BUSARA HATA KIDOGO KWA KOCHA WA AINA YAKE KUINGIA KWENYE MAMBO YA KISHABIKI KUKANDIA TIMU PINZANI TABIA HIYO HAIKUJENGEI SIFA NZURI KWA JAMII. HAYUPO MCHEZAJI ALIYESHIBA PESA NA WALA SI KILA MCHEZAJI ANATAKA KULIPWA DAU KUBWA NDIPO ASAJILI TIMU FULANI MFANO MZURI YANGA WENYEWE MNAO WACHEZAJI KAMA AJIBU, FEI TOTO, TSHTSHIMBI, MAKAMBO,YONDANI, GADIEL, THAMANI YAO YA KULIPWA KIUKWELI KABISA NI KUBWA SANA KULIKO WANACHOLIPWA LAKINI MAPENZI YAO NDANI YA YANGA WAMERIDHIKA.

    ReplyDelete
  5. SIMBA NI KAMPUNI , MO KAWEKEZA BILIONI 20 ITASHINDWAJE KUMLIPA MCHEZAJI MILIONI 39 . LICHA YA HUYO HATA MO SALAH TUKIMHITAJI ANAWEZA KUTUA MSIMBAZI NA SIKU HIYO HIYO ZAHERA ATAOMBA PO NA KUONDOKA BILA KUAGA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic