Kikosi cha Azam FC leo kimefanya mazoezi yake ya mwisho jijini Dar es Salaam ikiwa ni maandalizi ya mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City utakaochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Azam FC itamenyana na Mbeya City , keshokutwa, Jumapili ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa kikosi kipo sawa na wachezaji wana morali kubwa ya kutafuta ushindi.
"Tunawaheshimu wapinzani wetu tutawafuata kwa adabu kwa kuwa ni timu bora ila nasi pia tupo vizuri tunahitaji pointi tatu, mashabiki watupe sapoti," amesema Maganga.
Azam FC wapo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 30 wana pointi 63.
0 COMMENTS:
Post a Comment