April 12, 2019


KIKOSI cha Simba kimetia timu salama nchini Congo na kufanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wa kesho wa marudio wa hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Mchezo wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa, timu zote zilitoshana nguvu hivyo kesho kila timu inahitaji ushindi ili kupenya hatua ya nusu fainali.

Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kwa maandalizi ambayo ameyafanya kikosi kipo tayari kupambana na TP Mazembe.

" Tupo tayari kwa ajili ya kupambana kupata matokeo mchezo wa kesho na kutakuwa na mabadiliko kidogo ya kiufundi kwenye kikosi kwa lengo la kupata matokeo chanya," amesema.


Mchezaji Pascal Wawa ambaye ni beki ataukosa mchezo huo kutokana na kutokuwa fiti baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic