April 14, 2019


KOCHA Mkuu wa JKT Queens, Ally Ally amesema kuwa amebakiza mechi tatu kushinda ili atangazwe kuwa bingwa wa ligi ya wanawake Tanzania inayodhaminiwa na bia ya Serengeti.

Akizungumza na SportXtra, Ally alisema kuwa mpaka sasa hajaona kikosi chenye uwezo wa kumtingisha kutokana na kasi ya washambuliaji wake kuwa na uchu wa kufumania nyavu wawapo uwanjani.

"Kwa sasa nimebakiza mechi tatu kucheza kisha nitangazwe kuwa bingwa ninajiamini na ninawaamini wachezaji wangu tutashinda mechi zote na kuurejesha ubingwa.

"Hakuna anayetutisha kwa sasa ndio maana ukiangalia idadi ya mabao ambayo tumefungwa haitishi kama idadi ya mabao ambayo tumefunga, tumefunga mabao 82 na kufungwa mabao matatu pekee," alisema Ally.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic