April 22, 2019


WIKI hii ya Sikukuu ya Pasaka haikuwaacha salama baadhi ya mashabiki ambao wanazipa sapoti timu ambazo hutumia jezi nyekundu kwani asilimia kubwa nyingi zilichemsha na kuacha furaha kwa wapinzani wao.

Kwenye ligi ya Tanzania Simba ambao hutumia uzi mwekundu mara nyingi wakiwa nyumbani, walianza kupoteza mbele ya Kagera Sugar uwanja wa Kaitaba kwa kufungwa mabao 2-1.

Simba walionja joto ya jiwe Kaitaba kwani ndani ya dakika 90 walipiga mashuti matatu yaliyolenga lango huku wapinzani wao Kagera wakimlenga mara sita Aishi Manula.

Pia mashabiki wa Manchester United hawakuamini macho yao walipopokea kipigo cha kwanza kikubwa tangu meneja mpya Ole Gunnar apewe mkataba kwa kufungwa mabao 4-0 mbele ya Everton.

Manchester United ambao nao hutupia uzi mwekundu nao walikuwa na sikukuu ya Pasaka ngumu kidogo kutokana na timu yao kuzidiwa kila idara kwani ndani ya dakika 90 walipiga shuti moja tu lililolenga lango huku wapinzani wao wakipiga mashuti nane yaliyolenga lango.

Kwa timu ambazo hutumia rangi nyekundu ni Liverpool pekee ambao walikuwa wababe baada ya kufanikiwa kubeba pointi zote tatu kwa ushindi wa mabao 2-0 mbele Cardiff City.

Ushindi huo unawarejesha kileleni mwa Ligi Kuu Engaland wakiishusha Manchester City yenye michezo 34 na pointi 86 huku wao wakiwa wamecheza michezo 35 na pointi 88.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic