NA SALEH ALLY
KWANZA lazima tukubali Simba walikuwa na kila sababu ya kuhoji kuhusiana na uamuzi wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kuamua kuadili mwamuzi.
Caf wamembadili mwamuzi Bamlak Tessema Weyesa kutoka Ethiopia bila ya kutoa sababu za kutosha na badala yake nafasi yake imechukuliwa na mwamuzi Janny Sikazwe wa nchini Zambia.
Mechi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika Hatua ya Robo Fainali kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka katika nchi hizi mbili, yaani Tanzania na DR Congo.
Pamoja na hivyo, mechi hiyo inaendelea kuwa maarufu sana kwa kuwa inaikutanisha timu ambayo inaonekana kupata sifa ya “Kiboko cha Vigogo” hasa inapocheza nyumbani kwao dhidi ya mmoja wa vigogo wa Afrika.
Simba inaonekana inapokuwa nyumbani kwake Dar es Salaam, hakuna nafasi kwa timu yoyote hata kama ni kubwa vipi, na imeweza kudhihirisha hilo huku ikiibuka na ushindi dhidi ya vigogo kama Al Ahly, AS Vita na Mazembe wamekuwa timu pekee ambao hawakupoteza mchezo.
Wakati Mazembe walitua Dar es Salaam wakiwa wanajiamini sana, hakuna ubishi kwamba wameondoka na hofu kutokana na walichokiona kutoka kwa Simba ambao pamoja na sare ya bila kufungana, uchezaji wao ulionyesha ni timu hasa ambayo inaweza kupambana.
Sasa mwamuzi kutoka Ethiopia kama alionekana ni wa Afrika Mashariki na anaweza kuwa na undugu na Simba, vipi mwamuzi kutoka Zambia ambayo ni pua na mdomo na Lubumbashi? Yote ni ya kujiuliza lakini halipaswi kuwa na nafasi kubwa sana utafikiri hayo ndio maandalizi.
Simba wana kila sababu ya kuzungumza na tayari wameshafanya hivyo, inaweza ikawa ni sehemu ya tahadhari lakini viongozi hawapaswi kuendelea kulizungumza hilo hadi kufikia hali ya kujiondoa relini.
Nasema hivyo nikiwasisitiza kuwa makini kwa kuwa kama wataendelea hivyo, mwisho hili linaweza kuingia kwenye vichwa vya wachezaji wanoaweza kuanza kuamini kama wamekuwa wanaonewa na mwisho wakawa na mechi mbaya.
Wachezaji wanaweza wakawa wamelisikia hilo na wanachotakiwa ni kuwaachia wahusika washughulike na suala hilo halafu wao wakaendelea na kazi yao ya kucheza mpira na kutafuta ushindi kwa sababu ya kikosi chao.
Uamuzi wa kubadili refa hauwezi kuwa jibu la Simba katika kipindi kilichobaki, wamesema wamesikika na ilikuwa sahihi kusema lakini sasa wanapaswa kutupa nguvu nyingi katika maandalizi yao ya mwisho kabla ya kuivaa Mazembe, kesho ikiwa nyumbani kwake.
Mazembe lazima watakuwa wanaendelea kujiandaa na tena itakuwa kwa nguvu kwa kuwa hawawezi kusema watakaa wanaisubiri Simba wakitegemea mchekea. Tayari wameishaona kazi si rahisi, hivyo watajipanga hasa kuhakikisha wanashinda.
Kama TP Mazembe watakuwa wanajipanga vilivyo, vipi Simba waone suala la refa ni kubwa sana? Huenda lilifanyika makusudi kuwavuruga maana walijua pale atakapotangazwa mwamuzi lazima Simba wataekeleza nguvu kwenye kulalamika.
Hata kidogo Simba hawapaswi kuingia katika mtego huo na badala yake wapambane kuyafanyia kazi matatizo ambayo yanawafanya waonekane kama wanayumba. Waanzie katika safu ya ulinzi kuhakikisha wanacheza vizuri na kubadili mambo.
Simba wamekuwa hawajiwezi katika ulinzi wanapotoka nje ya nyumbani. Angalia ndani ya mechi tatu wamefungwa mabao 12 ya ugenini. Kama watashindwa kuibadili hii, basi watakang’olewa bila hata ya ubishi.
Wakikomaa na hilo, basi wanaweza zaidi kuleta mapinduzi kwa kufanya kile ambacho hakikuwa kimetarajiwa na wengi.
Wachezaji waendelee kujikita katika kile kinachoaminika ndiyo kinahitajika kufanyika ili kuisaidia Simba kuing’oa Mazembe badala ya wao kutumika kama sehemu ya kujiangamiza.
Kuelekea mechi za quarter finals za champion league jumamos Alahly ya Egypt imedhamiria kuivunja rekodi ya Simba kesho pale Borg Al Arab kwa kupindua matokeo ya goli tano bila za mamelody Sundown ya Africa kusini. Mpaka sasa Simba ya Tanzania ndio inayoshikilia record ya kupinndua matokeo baada ya kupoteza mchezo kwa goli nyingi. Simba ilifungwa goli nne mzunguko Dareslaam 4:0 na Mufurira wanderas ya Zambia.Lakini kwenye mechi ya maruduano ugenini Zambia Simba ililipiza kisasi kwa kuibamiza timu hiyo ya Zambia kwao goli tano mtungi 5:0. Kiuhalisia hata Alahly akipindua matokeo ya mamelody itakuwa bado hajaivunja rekodi ya Simba kwani Simba wao walipindua matokeo hayo ugenini na hii inaonesha kwa jinsi gani Simba ilivyo na historia ya aina yake kwenye mashindano ya klabu bingwa Africa. Kuelekea mchezo wa kesho na Mazembe, wachezaji wa Simba licha ya mafundisho na maelekezo ya kocha wao lakini wao wenyewe wanatakiwa ndani ya nafsi zao kuwa na nia ya kujitoa kwa silimia 100. Na hasa kuwa makini kwa kiwango cha asilimia 1000 katika ndani ya kipindi cha kwanza hasa dakika za mwanzoni za mchezo. Mazembe watauanza mchezo wa kesho kwa vishindo ili kupata goli la mapema la kuwanyanganya Simba ili kuimaliza Simba mapema na kamwe Simba wasikubali kumrahisishia kazi Mazembe kesho kwa kuanza mchezo kwa staili ya ulegelege. Kutakuwa na matukio ya ajabu kabla nadani ya mchezo ili kuwatoa Wachezaji mchezoni ila wao hawana haja ya kuhofu kitu ni kuzingatia nidhamu na kufokasi na mchezo wenyewe kwa vitendo.wachezaji wanatakiwa kuwa makini sana katika mchezo wa kesho muda wote na wanatakiwa kupambana hasa na ikitokea kupoteza mechi basi lazima waache alama zao Congo na isiwe kukubali kupoteza mechi hivi hivi tu kirahisi rahisi. Vile vile wachezaji wa Simba wanatakiwa kupiga mashuti golini yenye shabaha hasa ya mbali kila nafasi zitakapopatikana na kuacha kupoteza muda mwingi kupiga square passes . Kwa jinsi mechi itakavyokuwa hapana shaka Mazembe watajiimarisha sana kwenye ulinzi ili kutoruhusu Simba kupata goli la ugenini na kwa kuelewa hilo wachezaji wa Simba lazima wawe na malengo ya kimkakati maulumu ya kujaribu mashuti ya mbali yanayolenga goli na hapana shaka kwenye nia basi pana njia pia na Mungu atawaongoza.
ReplyDeleteKila la kheri Simba.
Simba hawana jipy wanadhan Kila wanapocheza na tp mazembe watawatoa kwa kuwakatia rufaa,ahahaaaa muwaambie Safari hii hayupo tena bukungu,sisi km wayanzania tunawapongeza kwa hatua mliyofikia lkn et mkawatoe mazembe mnatafuta tu sababu kwamba et mlibadilishiw refa huo ni ufinyu wa mawazo mtapigw tu
ReplyDeleteumeshachangia bakuli la timu yako au unakuja kupiga kelele tu hapa
Delete