KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kupambana na kubeba pointi tatu mbele ya Yanga kesho Uwanja wa CCM Kirumba.
Kagera Sugar haijawa na mwenendo mzuri msimu huu kwani imepoteza michezo miwili mfululizo kwa kuanza ule uliopigwa uwanja wa Nyamagana dhidi ya Azam FC na uliopigwa uwanja wa Namfua dhidi ya Singida United.
"Najua utakuwa mchezo mgumu na wenye kasi ila tutapambana kupata pointi tatu muhimu kwani matokeo yetu yamekuwa si ya kuridhisha, tunaiheshimu Yanga ila hatuna hofu nayo," amesema Maxime.
Kagera Sugar ipo nafasi ya 17 ikiwa na pointi 36 ikiwa imecheza michezo 31.
0 COMMENTS:
Post a Comment