NA SALEH
ALLY
TANGU timu ya
taifa, Taifa Stars ifanikiwe kushinda nafasi ya kucheza katika Kombe la Mataifa
Afrika (Afcon), kwa mara ya pili, kumekuwa na muunganiko mkubwa wa Watanzania
kupitia kila nyanja na muunganiko mkuu ukabaki kwenye michezo na hasa soka.
Kama
unakumbuka, wasanii wa muziki, uigizaji nao walishiriki katika hamasa na ndio
maana unaona muunganiko wa wapenda michezo na soka, wale wa burudani ukafanya
Uwanja wa Taifa ushindwe kuhimiliki vishindo baada ya watu kukosa nafasi siku
mechi ikipigwa.
Muunganiko
huu, umefanya mchezo wa soka uendelee kuwa gumzo wakati Tanzania ikielekeza
tena macho yake katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali
wakati Simba inakwenda kuivaa TP Mazembe kesho Jumamosi.
Gumzo la
mechi hiyo nalo limekuwa kubwa, kila upande ukionyesha nia ya kufanya vema,
lakini muigizaji Steven Mengere anaonekana kuchafua hali ya hewa.
Siku chache
zilizopita Mengere maarufu kama Steve Nyerere alikuwa akihojiwa na kituo kimoja
cha runinga ya mtandaoni. Alizungumza mambo kadhaa kuhusiana na soka lakini
kuhusu Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara.
Steve
Nyerere hakuishia hapo, alisonga zaidi hadi kwa mashabiki wa Simba ambao hakika
aliwakosea heshima, jambo ambalo hatupaswi kuacha lipite hivi maana litakuwa
funzo linalotuzuia kukosea kwa mara nyingine.
Alieleza
jambo zuri, kwamba atawaunga mkono Simba dhidi ya TP Mazembe na watashirikiana
kuhakikisha wanashinda licha ya kwamba yeye si Simba. Hili ni jambo zuri kwa
kuwa zaidi anaonyesha ni mzalendo.
Maneno haya
ya Steve Nyerere yanaweza kubaki kuwa mfano mzuri hata hapo baadaye na
kuonyesha kwamba alikuwa tayari kuishangilia Simba wakati yeye si Simba lakini
ni kwa sababu ya uzalendo, hivyo wasio wazalendo wabadilike.
Baada ya
hapo, Steve Nyerere aliulizwa kuhusiana na Manara, alichokisema kuhusiana na
Manara kuwa ni mtu wa hovyo kwangu naona si kitu kibaya kwa kuwa zaidi ni utani
wao ambao naujua unaendelea mara kwa mara kwa kuwa ni maswahiba.
Alichokosea
ni pale alipotumbukia katika suala la mashabiki akiwazungumzia wale wa Yanga na
Simba. Baadaye akasema anajua Watanzania idadi yao ni milioni 57 (hatujui
alikoitoa). Akasema mashabiki wa Yanga wako milioni 39, lakini Simba wako
milioni 3.4 na kati ya hao mashabiki wa Simba, mashabiki milioni 2.1 ni
Waarabu.
Hii maana yake
nini, Waarabu si Watanzania, hawapaswi kuwa mashabiki? Timu yenye mashabiki wa
aina hiyo si ya Tanzania? Hakika ni jambo baya sana kuzungumzwa na mtu
anayejitambua na hasa kwa mtu kama yeye Steve Nyerere ambaye anaonekana ni kama
kiongozi na ameshiriki kwenye uongozi hadi wa Bongo Movie.
Maana yake,
Waarabu si watu? Hawana haki ya kushangilia mpira? Wakiwa katika timu wanapaswa
kugawanywa kwa idadi yao? Kinachosikitisha zaidi, maneno ya kibaguzi
anayoyatoa, yalipigwa vita sana mwanzoni na Mwalimu Julius Nyerere ambaye yeye
sasa anatumia jina lake bila ya kibali.
Huenda hili
watu wengi wameliona ni kama jambo la kawaida sana, lakini Steve Nyerere
anapaswa kuamka na wengine muangalie ujinga huu usije ukarudia wakati mwingine,
ni jambo baya sana kurejesha ubaguzi na tena michezoni.
Michezo
inaunganisha watu, inawafanya wengi wajisikie kuwa pamoja. Hivyo si sahihi
kuanza kuzungumza maneno makali na mabaya kwa kigezo cha utani, yaani alikuwa
akimtania Manara. Vema kuangalia wakati wa utani ni wapi au kipindi gani.
Kiungwana
Steve Nyerere kama anaamini uungwana ni vitendo na uanadamu bora basi anapaswa
kuwaomba radhi wale ambao anaamini ni Waarabu aliokuwa akiwataja.
Pia
nimsisitize licha ya kwamba ni rafiki yangu na tunaheshimiana, lazima awe
makini na maneno anayozungumza maana mbeleni anaweza kukwama katika ndoto
anazotaka kuzitimiza kwa watu kumkumbusha maneno au matendo ya kijinga
aliyoyafanya kabla.
Usimlazimishe mtu kuipenda Simba.... Ila yeye ni mtazamo wake hayo mengine unaongezea wewe.... Wewe mbona huwa unatuongopea humu.....wewe ni mshabiki wa simba.... Usitulazimishe
ReplyDeleteUsimlazimishe mtu kuipenda Simba.... Ila yeye ni mtazamo wake hayo mengine unaongezea wewe.... Wewe mbona huwa unatuongopea humu.....wewe ni mshabiki wa simba.... Usitulazimishe
ReplyDeleteUnaona ujinga wa nyerere tu huo ujinga wa manara kuwasema wakongo nisawa acha moyo uende upendapo
ReplyDeleteChangia point, Alilosema hata mimi sijalipenda ni ubaguzi ambao si mzuri, unajenga chuki na ubaguzi ndan yake. Msanii ni kioo cha jamii unapooongea kitu jiulize mara mbili na uangalie na athari zake
ReplyDeleteKwani hapa Tuko Congo?
ReplyDeleteSareh wewe ni mmbea sana mbona hakuna issue hapo. Steve yuko sahihi ila ww ndo unakuza mambo.
ReplyDeleteAombe radhi,tukiendekeza mihemukobya kishabiki bila kujua shabaha ya uzalendo wetu, leo uarabu tunaukalia kimya,kesho tutaingiza uchaga,uzinza,ujita,uhehe.aombe radhi.
DeleteUjinga wa Manara huoni eeee,,,,umeumia kwa Hilo wee poleni Sana ila ndo ukweli huo nyie mijitu mweusi mnajipendekeza Tu kushabikia simba
ReplyDeleteSaleh hakika wew c mwandishi bali mnazi tuu ,next time tumia cerebrum vizuri
ReplyDeleteMashsbiki wote wa Manchester United ni Wazungu? Mashsbiki wote wa Liverpool ni wazungu? Mashabiki wa Buyern Munich ni wajerumani au wazungu? Mashsbiki wote wa Barcelona ni waspania? Mashsbiki wote wa real Madrid ni waspania? Pengine wewe mtanzania povu linakutoka kwa Manchester United yako hata huko uengereza unakusikia jina tu vipi leo unakwenda kumzodoa mtanzania kwa maneno ya kipumbavu na Simba yake ya Tanzania? Salehe Jembe yupo sahihi kabisa kulileta hili jambo na tunapaswa kulikemea kwa nguvu zetu zote. Huwezi kuzungumza au kuunga mkono ujinga wa maneno ya kibaguzi ya kipumbavu kama aliyoyazugumza Steve Nyerere juu ya mashabiki wa Simba kama wewe mwenyewe si mpumbavu na msenge wa akili. Kufulia kwa Yanga isiwe nongwa ya kuitakia mabaya Simba vile vile. Mashsbiki wa Simba na Simba yao watabakia kuwa Juu Tanzania na roho mbaya kamwe haijengi kitu na ndio maana migogoro haindoki upande wa pili. Hasada sio kitu kizuri hata kidogo watanzania tuachanane na maneno ya chokochoko ya kibaguzi.
ReplyDeleteDu hivi kumbe yanga hayurusu watu wenye asili ya nje but watanzania hakuna kushabukia hii timu,huyu mnaye mlilia kila siku ni black kanjibay
ReplyDeleteKWANI TATIZO NINI ? WAARABU? AU WAHINDI? ACHENI UBAGUZI USIO NA MAANA. YANGA KUNA BIN KLEB, KUNA YULE MKUU WA SPOTI PESA WALE NA HAO WA SIMBA TOFAUTI ZAO NINI? MANJI MZARAMO? ACHENI UPUUZI WA KUBAGUANA KWA RANGI, MATAIFA,MAKABILA AU UDINI. HUYU JAMAA AAMBIWE THATS TOO LOW.
ReplyDeleteAnaeona steve yupo sawa atakua ana matatizo. Hiyu jamaa huwa simwelewi ni nani kwenye taifa maana kama uigizaji hajui anachojua michango ya misiba tu huyu hana lolote
ReplyDelete