April 5, 2019


Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Keissy leo asubuhi ameomba mwongozo kwa Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson akiwataka wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania kuichangia klabu ya Yanga.

Keissy ametoa ombil hilo akisema anataka waichangie Yanga kwa kukatwa fedha 50,000 hadi 100,000 kwenye posho zao za leo ili kuisaidia klabu ya Yanga ila hoja hiyo ilipigwa chini na wabunge wengi.

Baada ya hoja yake kukataliwa na wabunge wengi, Keissy ameitaka serikali waiingize klabu ya Yanga kwenye mpango wa mfuko wa maendeleo ya Jamii (TASAF).

Amefuguka kwa kuitaka serikali iingize Yanga kwenye mfuko huo unaofanya kazi kusaidia kaya maskini ili wapatiwe msaada ambao utawasaidia kujinasua kwenye ukata wa fedha unaoikabili klabu hiyo.

4 COMMENTS:

  1. Huyu jamaa mbona maneno yake hayaingii Kama kweli anaipenda timu hiyo basi yeye awe mdano kujitolea mshahara wake. Hapo ni bungeni sio club ya yanga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. YEYE NI SHABIKI MKUBWA WA SIMBA ILA ANA MOYO WA HURUMA KWA YANGA

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic