April 5, 2019


Aliyoyazungumza Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji Mo kuelekea mechi ya kesho na TP Mazembe.

"Tumejipanga vizuri sana, ari ya wachezaji wetu ni kubwa na Mungu akitujalia basi kesho tutafanya maajabu. Mimi kilichonileta hapa ni kuwaomba mashabiki wa Simba, Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani"- Mo Dewji.

"Kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, moja unawaongezea nguvu wachezaji wetu na wao wanaona kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inawaogopesha wapinzani wetu"- Mo Dewji.

"Niwashukuru mashabiki wa Simba, niwapongeze ukiangalia takwimu za mechi za Ligi ya Mabingwa hakuna timu ambayo imejaza uwanja wake kama Simba Sports Club, Simba inaongoza kwa kujaza uwanja kwenye mechi zake"- Mo Dewji.

"Nawaomba sana mashabiki ikitokea bahati mbaya ya hapa na pale, tuendelee kushabikia sio tu mpaka tukipata goli, naomba sana tubadilike kwenye hilo, tushangilie Simba tangu mwanzo hadi mwisho"- Mo Dewji.

"Hapa hatushiriki tu, tunajiamini kwamba tunaweza na tunataka kwenda mbali zaidi ya hapa"- Mo Dewji.

"Shabaha yetu sio tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu"- Mo Dewji.

4 COMMENTS:

  1. Akili kubwa ni akili kubwa tu..Jamaa MO anaongea vizuri sana tena kwa ustaarabu usio kifani...
    Ila sasa ngoja aje Manara atabwabwaja weeeh hadi mwisho anaishia kuwakwaza hao hao wachezaji na mashabiki ambao Simba inawahitaji..!!

    ReplyDelete
  2. MO kasema ya moyoni...
    Ukweli ni kuwa mashabiki wengi wa soka la Bongo wana shabikia na kusapoti timu zao wakiona goli, tiktak, dobo, kanzu au chenga zenye maudhi.. Tofauti na hapo watakuwa kimya kama wapo msibani..
    Kwa wingi wa wanaoenda viwanjani.. nadhani tubadilike na kuzipa sapoti timu zetu muda wote wa mchezo.. wawe nyuma au mbele.. wamezidiwa au hawajazidiwa.. muda wote kuwepo na amsha amsha za maana yaani..!!
    #Ile ni Ile na Hii ni Hii..

    ReplyDelete
  3. Kukiwa na watu sahihi katika nafasi sahihi siku zote mambo hayawezi kuyumba. Pesa peke yake haitoshi kuonyesha uwezo wa mtu bila ya uwepo wa busara, hekima na unyumbulifu wa mambo (Uwezo wa akili kungamua mambo na kuyachanganua).

    MO ni mtu sahihi (Siwezi kusema tu kwa klabu ya Simba). Ameongea maneno machache sana kwa muda mfupi sana, lakini iwapo Wana-Simba wote tutayafanyia kazi, hususani yanayohusu siku ya kesho, basi huo muda mfupi alioutumia kuzungumza hayo maneno machache, utakuwa na faida kwetu wana-Simba, Tasnia ya Mpira wa miguu na Taifa kwa ujumla, kwa muda mrefu sana huko mbele.

    Binafsi, nimeyapokea kwa heshima na taadhima kubwa maneno yake, nitayafanyia kazi kwa nafasi yangu, nakuomba nawe mwenzangubila kujali ni mshabiki wa timu gani, tuungane kesho (Kwasasa Simba ni Yetu Sote).

    ReplyDelete
  4. Tofauti inaonekana dhahiri kuwa waliowekeza kwenye fedha na timu bora matokeo yanaonekana uwanjani....Simba imekuwa mfano kwenye uwekezaji pia Azam (ambaye alianza siku nyingi) na pia mtaji wa ziada wa Simba ni nguvu ya mashabiki....sasa Yanga watakewasitake lazima watafute wawekezaji wa hali ya juu (makampuni kama Subway, Chinese Companies) kumzidi Mo kwakuwa nao pia kama ilivyo Simba wanamtaji wa mashabiki ila sasa hivi hawajitokezi kutokana na kwamba kikosi chao hakivutii hakina wachezaji wenye kiwango cha juu na hata benchi la ufundi sio la kiwango cha juu....mabadiliko ni lazima ili upate support ya fans lazima uwe na kikosi imara

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic