April 26, 2019






NA SALEH ALLY
HATUWEZI kuwa na timu ambayo zinapendelewa halafu tukafanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa. Kama tutakuwa na ligi yenye kiwango sahihi, basi tuna kila sababu ya kuwa na timu imara.


Kama Ligi Kuu Bara ina timu 20, tunaamini kumekuwa na ushindani mkubwa katika mechi nyingi hasa zile zinazoonyeshwa kwenye runinga ya Azam TV ambayo tunapaswa kuipongeza kwa kuleta mabadiliko makubwa kwenye mpira wa Tanzania baada ya mechi nyingi kuanza kurushwa moja kwa moja.


Umesikia watu wengi ambao ni wadau wa karibu kama wachezaji, makocha na kadhalika wamekuwa wakisema kuwa mechi nyingi zinazoonyeshwa moja kwa moja huwa hazina upendeleo.


Wanasema mechi nyingi zisizoonyeshwa, timu wenyeji wamekuwa wakipewa upendeleo wa wazi kuhakikisha wanabeba pointi za nyumbani maana yake si kwa uwezo wa mpira, jambo ambalo ni bayana linaudumaza mpira wa Tanzania ambao tunaupigania kukua.


Ili soka likue, lazima liwe na haki na nafasi kwa watu kuchezeshwa kwa haki, haki itawale na kutengeneza uimara unaotokana na ushindani sahihi kabisa.


Nimeamua kuandika makala haya baada ya kuona kuna kampeni ya chinichini ambayo haina faida kwa mpira wa Tanzania na inaonekana tumekuwa tunaoneana haya kwa kisingizio cha fulani shabiki wa timu fulani.


Kampeni za kusema Simba inapendelewa, Simba imekuwa ikipewa nafasi ya kushinda na kadhalika. Lakini wanaosema wamekuwa hawana uthibitisho wa zaidi ya asilimia 90 wa wanayoyasema.


Kinachoshangaza ni kuona na watu wengine ambao hawajaribu kutafakari yanayozungumzwa, wanayachukua na wao kuyazungumza kutoka kwa waliyoyasikia bila sababu au hoja sahihi.


Simba inapendelewa katika mechi ipi, kama imefunga mabao halali, vipi inapendelewa. Kuna bao ilipendelewa, jibu hapana, ila ilichezeshwa saa 8 badala ya saa 10 kama ilivyoelezwa. Kwani aliyecheza naye alicheza saa ngapi, naye alicheza muda huo pia. Sasa kupendelewa kunatokana na nini hasa?


Sote tunajua, Simba ndio wana timu bora kabisa katika Ligi Kuu Bara kwa msimu huu na hili linadhihirishwa na takwimu zao kwa maana ya wastani lakini hata hatua waliyofikia kimataifa na kuitangaza Simba mbali barani Afrika.


Pamoja na hivyo, unaona Simba iliyoifunga Al Ahly, AS Vita, JS Saoura na kutoka sare na TP Mazembe, imekwenda kufungwa kwa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar ambayo inapambana kuepuka kuteremka daraja katika Ligi Kuu Bara!


Hapo unaweza kujiuliza, kwamba kama ni hivyo, Simba inayopendelewa inafungwa vipi na Kagera Sugar, inahenyeshwa vipi na KMC lakini kabla ya hapo tuliiona ikipata shida kubwa dhidi ya Coastal Union pale Tanga.


Wanaofanya kampeni za kutengeneza lawama ni kampeni chafu na za kipuuzi, kampeni zinazoonyesha wameshindwa kufanya kazi zao na baada ya hapo wanasambaza maneno yatakayowalinda siku wakianza kuhojiwa kutokana na kufeli majukumu waliyokabidhiwa.


Kwa wale mnaosikia, vipi uamini vitu tofauti na ambavyo unaviona. Mtu hadi akuaminishe tofauti wakati na wewe uliona kabisa kila kitu kilivyo, vipi mtu mwingine akuaminishe tofauti na wewe uamini.


Wanaosambaza kile kisicho sahihi, vizuri kuwahoji kwa hoja badala ya kukubali kubeba wanachokisema hata kama ni pumba na kukisambaza pia.


Hatuwezi kuwa tayari kuona timu moja, mfano Simba inapendelewa halafu tukakaa kimya. Lakini kama si hivyo, basi mimi sitakaa kimya ili suala la mechi zinazochezwa tujadili mambo ya msingi na si haya ya kubabaisha kutokana na kuwapinga wanaobabaisha mambo.


Pia haitakuwa sahihi kuwasikia Simba sasa nao wakisema Yanga wanapendelewa baada ya ndani ya mechi tatu, kupoteza na kushinda moja wakati matarajio ilikuwa ni kushinda zote.


Tuache mpira uchezwe na kama kuna malalamiko yawe ya msingi badala ya kusambaza upuuzi.

14 COMMENTS:

  1. Ni kawaida ya yule ambaye hafanyi vizuri kulalamika pale anapona hafanikiwi..Hata Simba mwaka juzi walikuwa wananalalamikia saana maamuzi ya marefa na baadhi ya magoli Yanga walikuwa wakifunga.hiyo ni pamoja na TFF kutupilia mbali rufaa ya Simba juu ya Kagera kuchezesha mchezaji mwenye kadi tatu.Na TFF hawakutaka kabisa kuongelea kadi tatu...bali walisema ghalama ya kukataa rufaa haikulipwa..Yanga kama ilivyokuwa Simba mwaka juzi wafanye kila kinachowezekana Ili kupata point tatu na ikitokea bingwa akipatikana kwa tofauti ya goli basis iwe hivyo.Lipa wachezaji stahiki zao ili kuzuia mgomo..Ukikiria kama wako kwenye mgomo unaweza tabiri nani atashinda Jtatu.Sasa Simba ni kati ya timu nane bora Afrika .Je kufika hapo wamebebwa na CAF?Unalalamika kunyimwa goli dhidi ya Mtibwa...haya hata kama Yanga wangepewa like goli..wangepata point moja Je wangesogea mbele kiasi gani kwenye ubingwa? Au Simba wangenyimwa ile penalty ya KMC wangerudi nyuma kiasi gani?

    ReplyDelete
  2. Kampeni hii ilianzishwa na Zahera baada ya timu yake kupoteza mwelekeo. Akanyamaziwa ndio matunda yake tunayaona.

    ReplyDelete
  3. Kuhusu njama za Canavvaro eti alishiriki kuihujumu Yanga dhidi ya Simba!Mtu unajiuliza mechi ilichezwa tarehe 16 Februari 2019!Kwanini malalamiko yatolewe sasa?Hii timing inamfaidisha nani?
    Toeni ushahidi!Wacheni majungu kila timu ishinde mechi zake.

    ReplyDelete
  4. Hapa umeongea hoja za msingi; nimeuangalia mpira huu na kugundua kua wengi hata hao vyombo vya habari kama radio wanajiita wachambuzi lakini bado hawana uwezo wa kuchambua; wanamihemko, hawako fair na wengine wanaburuzwa tu, na wanaushabiki ndani yake. Mimi hua napenda simba ishinde kwa haki na sikupendelewa ila hua sioni wapi hasa wanapendelewa. Nahisi baadhi ya waandishi pia wawe wabunifu katika kutafuta habari za kuandika na sikutia shindikizo ili watu waamini kua kuna upendeleo au team flan inabebwa, haileti sura mzuri kwa baadhi wachambuzi wetu wakibongo wasiojua sanaa ya mpira

    ReplyDelete
  5. Ingekuwa bora kuwataja Kwa majina kinagaubaga ili wakome katika Fituna zao za kupalilia chuki

    ReplyDelete
  6. Waamuzi waliochezesha mechi ya Simba wamefungiwa....swali ni kwanini wamefungiwa?

    ReplyDelete
  7. SALEH ALLY UPO SAHIHI NA KWAKWELI UMEONGEA POINT. TFF CHUKUENI HATUA YA KUWAITA AKINA ZAHERA KWENYE KAMATI ZENU MUWAHOJI WAJE NA USHAHIDI WAKISHINDWA WAFUNGIENI MIAKA 2 WASIJIHUSISHE NA MPIRA

    ReplyDelete
  8. "Hapo unaweza kujiuliza, kwamba kama ni hivyo, Simba inayopendelewa inafungwa vipi na Kagera Sugar, inahenyeshwa vipi na KMC lakini kabla ya hapo tuliiona ikipata shida kubwa dhidi ya Coastal Union pale Tanga"

    Hivi kwani Yanga hizo mecha nne imepoteza ikiwa Dar?Kawaida mchezo huya ni mgumu kwa timu ngeni... Hata hao wote walioifunga simba 5-0 huks kwao, walipokuja Dar walikuwa dhaifu.Hivyo basi Simba kucheza chini ya Kiwango Tanga, Bukoba na Mwanza ni jambo linalotegemewa latina mpira!

    ReplyDelete
  9. juuko juz kati kampga mtu kigot cha kchwa kimya achana na madudu ya kambuz vs kmc kama offside ya erasto kumrudishia manula mpira

    ReplyDelete
  10. Muda mwingi Yanga wameutumia kuwa kwenye vyombo vya habari.....wakati Azam, Simba na timu nyingine muda wao mwingi wameuweka kwenye matayarisho na maandalizi ya mechi (kimwili na kisaikolojia).....sijui ni kwanini????Kocha Mwinyi Zahera wekeza muda wako kufundisha mpira....hiyo jumatatu sijui itakuwaje hapo jangwani baada ya mechi Azam vs Yanga?

    ReplyDelete
  11. Kwa nini waamuzi waliochezesha simba na KMC WAMEFUNGIWA.... UNAZI HUO WEWE

    ReplyDelete
  12. Kwa nini waamuzi waliochezesha simba na KMC WAMEFUNGIWA.... UNAZI HUO WEWE

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic