MAAMUZI MAPYA YATANGAZWA UNITED JUU YA DE GEA, WACHEZAJI WATANO WAPYA KUNUNULIWA
Tetesi za soka barani ulaya leo Alhamis
United kutomuuza de Gea
Klabu ya Manchester United imesema hawatalazimishwa kumuuza mlinda mlango David de Gea, raia wa Uhispania mwenye umri wa miaka 28, mwishoni mwa msimu hata kama watashindwa kukubaliana naye juu ya mkataba mpya, jambo linalochochea uwezekano wa kuwa huru kuondoka mwishoni mwa msimu ujao (Mirror)
Madrid wazidi kumnyatia de Gea
Real Madrid, Juventus na Paris St-Germain wote wanafuatilia kwa karibu hali ya De Gea . (Express)
Ole kununua watano wapya.
Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anataka kusaini wachezaji wapya watano. (Telegraph)
City wamuwekea mikakati ya kumsajili Niguez
Manchester United imejiunga katika mbio za kumsaka mchezaji wa Spain, Saul Niguez, mwenye umri wa miaka 24, huku Manchester City ikimchagua mchezaji mwenzake katika timu za Atletico Madrid na Spain anayecheza kama kiungo, Rodri Hernandez, mwenye umri wa miaka 22 kama mchezaji mbadala wanayelenga kumchukua. (ESPN)
Herrera kuondoka United
Kiungo Mspain Ander Herrera, akiwa na umri wa miaka 29, anaweza kuondoka Manchester United msimu huu baada ya kughadhabishwa na hali ya mkataba wake katika Manchester United. (Mail)
United yajiwekea matumaini kwa Odoi na Sancho
Manchester United wanaamini watawapata wachezaji wa England wa kimataifa, winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, akiwa na umri wa miaka 19, na winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, mwenye umri wa miaka 18, endapo watatakiwa kuamua kutoendelea kuchezea klabu zao ambazo zimeshikilia msimamo kuwa haziko tayari kuwauza . (Mail)
PSG na United zatuma ombi kwa Varane
Paris St-Germain na Manchester United wametoa ombi la awali kwa mlinzi wa Ufaransa anayechezea Real kwa sasa Raphael Varane, 25. (independent)
Schurrle na timu yake kushushwa daraja EPL
Mchezaji Mjerumani Andre Schurrle, mwenye umri wa miaka 28, atakua muathiriwa wa kwanza wa kushushwa daraja katika timu ya Fulham kwa kurudishwa Borussia Dortmund mwaka mmoja kabla ya muda wake. (Sun)
Everton waambiwa wawe tayari kumkosa Gueye
Everton wameambiwa wajiandae kuhama kwa kiungo wao wa kati Msenegali Idrissa Gueye ambaye sasa ana umri wa miaka 29 msimu huu . (Liverpool Echo)
Barcelona kuongeza mpunga kwenye akaunti yao
Barcelona inatarajia kupata kati ya euro milioni 250 na milioni 300 kwa mauzo ya wachezaji msimu huu ili kuongeza fedha kwenye akaunti za klabu na hivyo kuwa na uwezo wa kusaini mikata mipya bila kujihatarisha kifedha. (ESPN)
Kovacic ataka kubakia Chelsea
Kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, mwenye umri wa miaka 24, angependa abakie Chelsea, ambako anacheza kwa mkopo kuliko kurudi kwa klabu mama Real Madrid msimu ujao. (Goal)
Zabaleta abakiza miezi miwili West Ham
Mlinzi wa West Ham Pablo Zabaleta, mwenye umri wa miaka 34, anasema amebakiza michezo miwili kabla ya kuweza kutimiza kipengele katika mkataba wake ambacho kitampatia uwezo wa kusaini mkataba mpya wa kubaki katika klabu hiyo msimu ujao. (Newham Recorder)








0 COMMENTS:
Post a Comment