KOCHA wa timu ya Mbao FC, Salum Mayanga amesema kuwa leo lazima aikazie Azam FC iliyo chini ya kocha Idd Cheche ambaye amekuwa na mwenendo mzuri katika mechi alizocheza hivi karibuni.
Mayanga ambaye amekabidhiwa timu ya Mbao kutoka mikono ya kocha Ally Bushiri ameiongoza timu yake kwenye michezo miwili na yote amepoteza kwa kupokea kichapo alianza na mchezo wa kwanza dhidi ya Simba kwa kufungwa mabao 3-0 na mchezo wake dhidi ya Alliance FC kwa kufungwa bao 1-0.
"Nimeongoza timu kwenye michezo miwili na yote nimepoteza hii ni mbaya kwangu na kwa timu pia ila leo ni lazima nipambane kupata matokeo mbele ya wapinzani wangu Azam FC," amesema Mayanga.
Mbao wanaingia kwenye mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa kwanza kwa kuchapwa mabao 4-0 uliochezwa Uwanja wa Chamazi watamenyana kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
0 COMMENTS:
Post a Comment