April 7, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kesho wataingia tofauti kwenye mchezo wao dhidi ya African Lyon utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba ili kubeba pointi tatu.

Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kushinda kwa bao 1-0 kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Zahera amesema ni ngumu kupata matokeo kwa timu ambazo zipo nafasi ya chini kwenye msimamo hali iliyomfanya awape mbinu mpya wachezaji wake.

"Nimewaambia wachezaji wangu wanatakiwa wawape presha wapinzani wao muda wote mpaka kupata matokeo, mbinu yetu itakuwa ni kushinda mapema ili kuwa salama kwani tukianza kufungwa inakuwa ngumu kupata matokeo.

"Nimeona kwenye mchezo wetu dhidi ya Ndanda baada ya kufungwa mapema wapinzani wetu waliendelea kutushambulia jambo ambalo lilitufanya tukapoteza ila hilo tayari tumelifanyia kazi," amesema Zahera.

Lyon inashika nafasi ya 20 kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza michezo 32 na kujikusanyia pointi 22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic