April 26, 2019


MSEMAJI wa klabu ya soka ya Simba,  Haji Manara amemjibu Kocha  wa Yanga,  Mwinyi Zahera, baada ya kumhusisha Meneja wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, na kushindwa kwa Yanga katika mechi yake ya Ligi Kuu na Simba ambapo ilifungwa bao moja na mchezaji Meddie Kagere kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Gazeti la Championi Jumatano la  Aprili 24, 2019, liliandika kwamba Zahera  alisema yeye ndiye alimtimua  ‘Cannavaro’ baada ya kuonekana kwenye ofisi ya mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’,  licha ya yeye (Cannavaro) kufafanua kuwa alifika katika ofisi hiyo kwa ajili ya masuala yake binafsi.

Manara amemjibu Zahera kupitia mtandao wa Instagram akimataka athibitishe madai yake kwamba kitendo hicho cha Cannavaro kuonekana katika ofisi hizo kililenga kuwahujumu Yanga.

Ujumbe wa Manara ni ufuatao:

Leo  ”Kwa hili Zahera hatutakubali!!
Lazma uthibitishe beyond reasonable doubt kwamba Mwenyekiti wetu wa Bodi ya Wakurugenzi alishiriki kuwahujumu Yanga Kwenye mchezo wetu na nyie!!
Kocha usiye na heshma na unaeropokwa kila siku ili utafute kiki kwa Washabiki wa Yanga!! Lazma ujue MO ni mtu mwenye heshma kubwa ktk jamii na kumhusisha na vtu vya hovyo hovyo ,Simba haitakaa kimya ( no matter TFF hawakukemei hata siku moja)
Halaf unamtaja Canavaro ili umdhalilishe,yy ndio captain bora wa muda wote Yanga kafanya mambo makubwa pale na kashinda mataji mengi mno wakati ww hata kikombe cha Uji hujashinda hapo,nia ni kutaka uwe bora kuliko uliowakuta na ambao wamefanya mambo mengi pale!!!tumekuvumilia sasa imetosha,huwezi kila siku ukaituhumu klabu yetu halaf tukukalie kimya!! Sasa utaijua ukubwa wa Simba,labda ulikuwa ukiisikia tu 
Kesi hii nimeinunua kama Mkuu wa Habari wa Simba!!
Nikirudi nna ww ulete uthibitisho either TFF au Kwenye vyombo vya dola!!
Mpira hauwezi kuchezewa na watu wasiojielewa na kupayuka yuka”

5 COMMENTS:

  1. Jamani zahera mbona alishasema akikosa ubingwa asilaumiwe kwa sababu wachezaji alioambiwa kuwa wameshasajiliwa hawakusajiliwa? Mo ni mfanyabiashara na canavaro ni mjasiriamali wa muda mrefu sasa kuna shida gani hapo? Itafika muda mchezaji akipita mitaa ya msimbazi atafungashiwa virago. Zahera ana baahti moja tu yupo yanga ambayo inapitia kipindi kigumu vinginevyo 100% angeshatimuliwa.

    ReplyDelete
  2. HIVI SISI WANA YANGA TUKO SAWA CANNAVARO KUDHALILISHWA NA KOCHA NA KUSINGIZIWA TUNASAHAU MCHANGO MKUBWA WA CANAVARO? HATA KAMA CANAVARO ANGEONEKANA NA OKWI AU KAGERE ACHA HUYO MO OFISINI KWAKE, SISI WATANZANIA HATUNA CHUKI ZILIZOPITILIZA ZA NAMNA ZAHERA ANATAKA. SISI BADO TUNAISHI KINDUGU NA KIRAFIKI TUNAJITAMBUA NDIO MAANA HAJI MANARA SIMBA BABA YAKE MZAZI SUNDAY MANARA YANGA TENA MCHEZAJI KOMPYUTA WA YANGA KIPINDI CHAKE. KOSA LAKE NINI CANNAVARO? DHAMBI HATUIOGOPI?

    ReplyDelete
  3. Huyu zahera amekosa pa kutokea mwache tu

    ReplyDelete
  4. Muda mwingi Yanga wameutumia kuwa kwenye vyombo vya habari.....wakati Azam, Simba na timu nyingine muda wao mwingi wameuweka kwenye matayarisho na maandalizi ya mechi (kimwili na kisaikolojia).....sijui ni kwanini????Kocha Mwinyi Zahera wekeza muda wako kufundisha mpira....hiyo jumatatu sijui itakuwaje hapo jangwani baada ya mechi Azam vs Yanga?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic