UONGOZI wa Simba umempa kazi ngumu mlinda mlango namba moja wa kikosi hicho, Aishi Manula leo Uwanja wa Taifa kuhakikisha haruhusu bao hata moja kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya robo fainali dhidi ya TP Mazembe.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa leo Manula anatakiwa awaachie kazi ya kufunga washambuliaji nyota wa Simba wakiongozwa na Meddie Kagere ambaye ana mabao sita kwenye michuano ya Caf.
"Aishi Salum ni namba one (moja) wa nchi, ni kipa bora nchini kwa miaka mitatu mfululizo ni kipa wa Mabingwa wa Taifa hili.
"Unakwenda kudaka moja ya mechi za kihistoria kwako na moja ya mechi itakayoweza kukuweka katika daraja la makipa wakubwa Afrika.
"Aishi wewe ni shujaa tayari ila tunataka ujue utakuwa mkubwa mara mia kama utaondoka na clean sheet, kazi ya kufunga waachie kina Kagere na Bocco, kwako tunataka mikono yako ivae sumaku moyoni, watanzania na wanasimba tunakuamini," amesema Manara.
0 COMMENTS:
Post a Comment