April 22, 2019


Kiwango cha mshahara kumzuia Pogba kwenda Madrid

Kiwango cha mshahara anachokitaka kiungo wa Manchester United Paul Pogba kinaweza kikawa kikwazo kwa Real Madrid kumsajili nyota huyo raia wa Ufaransa. (AS)

Chelsea wampigia hesabu Coutinho

Chelsea wanapiga hesabu za kumnyakua kiungo wa Brazil na klabu ya Barcelona Philippe Coutinho, 26, kama mbadala wa mshambuliaji wao raia wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, ambaye mwisho wa msimu anatarajiwa kuhamia Real Madrid.(Calciomercato)

Man United kumpandisha cheo Phelan

Klabu ya Manchester United ipo tayari kumpandisha Mike Phelan mpaka kuwa mkurugenzi wa ufundi na nafasi yake ya Kocha Msaidizi kupewa kiungo wa zamani wa klabu hiyo Michael Carrick. (Mail)

Henry kutimkia Marekani

Mchezaji nyota wa zamani wa Arsenal ambaye pia alitimuliwa kwenye kazi ya ukocha na klabu ya Monaco Thierry Henry, yumo kwenye mazungumzo na klabu ya New York Red Bulls ya ligi ya soka Marekani ili kujiunga nao kama mkufunzi. (Sky Sports)

Mbappe akanusha kuhamia Madrid

Mshambuliaji nyota wa Ufaransa na klabu ya PSG Kylian Mbappe, 20, amekanusha uvumi ulioenea kuwa ana mpago wa kuhamia Real Madrid. Mbappe ametoa kauli hiyo baada ya kuifunga goli tatu timu yake ya zamani Monaco. (Goal.com)

Marcelo akana kwenda Juventus

Beki raia wa Brazil Marcelo amesisitiza kuwa hana mpango wa kuihama klabu yake ya Real Madrid mwishoni mwa msimu huu licha ya uvumi kuenea kuwa mchezaji huyo alikuwa akitammani kuungana tena na Cristiano Ronaldo katika klabu ya Juventus. (Bein Sports, via Mirror)

Kocha Aston Villa afutwa kazi

Kocha wa muda mrefu wa wachezaji chipukizi wa Aston Villa Sean Kimberley ameikacha klabu hiyo. (Birmingham Mail)

Benitez ataja mishahara kuwa sababu ya kuidhoofisha Newcastle

Bosi wa Newcastle Rafa Benitez amedai kuwa mfumo wa mishahara wa klabu hiyo unaifanya timu isiwe na matokeo mazuri kwenye Ligi ya Premia. (Newcastle Chronicle)

Imeandaliwa na BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic