April 22, 2019


BAADA ya Simba juzi kupokea kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems amewavaa wachezaji wake kwa kucheza chini ya kiwango.

Simba ilipoteza mchezo wake wa pili wa ligi msimu huu kanda ya ziwa kwani hata mchezo wa kwanza ilipoteza mbele ya Mbao FC Uwanja CCM Kirumba kwa kufungwa bao 1-0 na juzi ilipoteza mbele ya Kagera Sugar.

Aussems alisema kuwa wachezaji wake walishindwa kufuata maelekezo aliyowapa na walianza kucheza kama wameshinda ilihali wapo ugenini na aliwaambia awali kuwa mchezo utakuwa mgumu.

“Kabla ya mchezo niliwaambia wachezaji wangu kwamba mchezo utakuwa mgumu kutokana na hali ya kikosi ambacho wanapambana nacho kuwa katika nafasi za chini, hivyo ni lazima wangepambana kupata matokeo.

“Nilishangazwa na uwezo wa wachezaji kipindi cha kwanza, sikuona kazi waliyofanya, wote walikuwa wamepumzika kama hakuna kitu, ndiyo maana tulifungwa mabao yote kipindi cha kwanza ila kipindi cha pili ndio walishtuka na kurejea kwenye ubora wao, ila tumepoteza,” alisema Aussems.

Simba wamesimamishwa na Kagera Sugar na kubaki na pointi zao 60 baada ya kucheza michezo 24, Jumanne watakuwa kazini kumenyana na Alliance ya Mwanza katika mchezo mwingine mgumu wa Kanda ya Ziwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic