April 3, 2019


MBELGIJI wa Simba leo atakuwa kibaruani kumenyana na JKT Tanzania ambao kwa sasa wapo chini ya kocha mkuu, Mohamed Abdallah, 'Bares'.Leo ametangazwa kuwa kocha bora wa mwezi Machi. 

Aussems amesema kuwa ugumu uliopo kwa sasa ni kwenye ratiba kutokana na kucheza michezo mfululizo huku akiwa na kibarua cha kumenyana na TP Mazembe Jumamosi.

"Kikosi kipo sawa na tunatambua kwamba tunacheza na timu ngumu hilo halitupi mashaka tutapambana kutafuta matokeo ili kujiweka sehemu nzuri zaidi pia ratiba inatubana kwani Jumamosi tutacheza na TP Mazembe ila mpaka nimalize mechi hii kwanza," amesema Aussems.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye ligi imecheza michezo 22 ikiwa na jumla ya pointi 57.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic