April 13, 2019


BEKI Mganda, Joseph Ochaya, anayekipiga TP Mazembe, amewaonya Simba kuwa, wajipange kupokea kipigo kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa leo Jumamosi mjini Lubumbashi, DR Congo.

Wikiendi iliyopita, Simba walishindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani, katika mchezo wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulazimishwa suluhu.

Ochaya alisema kuwa walikuja Dar kuwasoma Simba na sasa wameshawajua, hivyo watakwenda kuwaonyesha kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa kwenye dimba lao.

“Sina mengi ya kusema, watu wasubiri tutakachokifanya kwenye mchezo wa marudiano, tumeshawajua Simba, hivyo hawatatusumbua kabisa,” alimaliza Ochaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic