April 8, 2019


Mchezaji wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania, Jonas Mkude, ametoa fedha taslimu shilingi laki tano kumsaidia mchezaji wa zamani wa Pamba ya Mwanza na Simba, Alphonce Modest kwa ajili ya matibabu.


Modest ambaye amezichezea pia timu za Yanga na Mtibwa Sugar, amekuwa akisumbuliwa na homa kwa muda mrefu.

Pia wachezaji wa zamani kupitia chama chao wametoa shilingi laki saba kumchangia mwenzao.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa baba yake Modest, mitaa ya Kinondoni jijini Dar Es Salaam.

Pichani juu Mkude anaonekana akiwa na baadhi ya wachezaji wa zamani; Mohamed Mkweche, Shaban Katwila, Athanas Michael, Mwenyekiti Paul Lusozi na Katibu Sebastian Mwendamaka.

Imeandaliwa na Zaka Zakazi

1 COMMENTS:

  1. Hongera sana mkude na mwenyezi mungu atakurudishia pale ulipotoa tunaomba na wachezaji wengine watakaoguswa na mwezao watoe kwa moyo. Kutoa ni moya tusisubili mpaka mtu afe ndo mkatoe rambirambi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic