KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa bara la Afrika hajaona timu yenye mashabiki wenye utofauti kama wa Yanga na anaamini iwapo wataichangia itatisha msimu ujao.
Zahera amesema kuwa kwa namna Yanga ilivyo kubwa ina hadhi ya kuwa ya kimataifa na kushindana kwenye makombe makubwa ndani ya bara la Afrika.
"Katika muda niliofanya kazi hapa, nimesoma na kujifunza vitu vingi sana. Hata kwa haya ninayoshuhudia kwa sasa, hakika msimu ujao hatutoumia.
"Nimetembea karibu nchi zote za Afrika nikiwa na timu ya Taifa, nawahakikishieni hakuna hata nchi moja yenye mashabiki kama hawa wa Yanga, hata TP Mazembe haina fanbase kubwa kama Yanga.
"Kuna ulazima gani timu kama hii eti kungoja tajiri mmoja aje awekeze pesa zake? wakati wenyewe mnasema hii ni timu ya wananchi? kwanini wananchi tusiibebe timu yetu wenyewe? sasa tunapaswa kuibeba wenyewe.Timu kama Yanga SC inapaswa kushindania makombe makubwa Afrika. .Naomba tuichangie Yanga," amesema Zahera.
0 COMMENTS:
Post a Comment