HATUA ya upangaji wa makundi ya michuano ya Afcon ya Afrika imepangwa leo nchini Misri ambapo tayari Tanzania imewajua wapinzani wake watakaomenyana nao mwezi Juni nchini Misri.
Hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania wakiongozwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Wallace Karia pamoja na Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Emmanuel Ammunike yalishuhudiwa na Dunia nzima kupitia SuperSport
Pia ilihudhuriwa na nyota wa zamani kwenye soka kama Mustapha Hadji mchezaji wa zamani wa AS Villa na timu ya Taifa ya Morrocco, Eliaj Diof mchezaji wa zamani wa Liverpool na timu ya Taifa ya Senegal, nahodha nstaafu wa timu ya Misri Ahmed Hassan, nahodha mstaafu wa timu ya Ivory Coast na timu ya Barcelona Yaya Toure.
Tanzania iliwekwa kwenye poti namba 4 lililokuwa na timu kama Zimbabwe, Namibia, Guinea Bissau, Angola na Burundi.
Huku Kenya ikiwa kwenye poti namba 3 lenye timu kama Afrika Kusini, Uganda,Benini, Mauritania na Madagascar.
Congo walikuwa poti namba mbili lilolokuwa na timu kama Ghana, Mali, Ivory Cost, Guinea na Algeria.
Wenyeji Misri wao walikuwa poti namba moja lililokuwa na timu kama Cameroon, Senegal, Tunisia, Nigeria na Morocco.
Porti namba nne lilikuwa ni la kwanza kuchanganywa na timu ya kwanza kuchaguliwa ilikuwa Zimbabwe
Kundi A
Misri
Zimbabwe
Uganda
DR Congo
Kundi B
Burundi
Madagascar
Guinea
Nigeria
Kundi C
Tanzania
Kenya
Algeria
Senegal
Kundi D
Afrika Kusini
Namibia
Ivory Coast
Morocco
Kundi E
Angola
Mauritania
Mali
Tunissia
Kundi F
Guinea Bissau
Benin
Ghana
Cameroon
Burundi, Madagascar, Maurtania ni mara ya kwanza kushiriki michuano ya Afcon hatua ya makundi.
0 COMMENTS:
Post a Comment