April 2, 2019


MSANII wa Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, anayesumbua kwa sasa na ngoma yake ya 'Your Are The Best' amesema kuwa katika maisha yake anapenda kusaidia jamii kwa kila anachoweza bila kumbania mtu yoyote.

Dimpoz amesema kuwa binadamu wanapaswa watambue kuwa duniani ni mapito na kusaidiana ni jambo la kheri kwa kila anayefanya hivyo bila kuwa na sababu ya kuwa na roho mbaya.

 "Katika maisha yangu siku zote sina roho ya kusema nimbanie mwenzangu kupata kitu kwani hata kama tungekuwa na ugomvi kiasi gani, pale ninapoona mtu ana uhitaji, kumsaidia huwa sina kinyongo.

"Imani yangu ni kwamba riziki ya mtu ipo popote hivyo sina ulazima wa kumbania mtu yoyote katika jambo lolote, naamini kwenye upendo na kujitoa," amesema Dimpoz.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic