April 9, 2019


Mchezo kati ya Simba Sc dhidi ya Bishara United ya Mara uliotakiwa kuchezwa leo katika uwanja wa Jamhuri Morogoro umehairishwa tena kwa kile kilichoelezwa ni kupisha maandalizi ya mechi kati ya Tp Mazembe dhidi ya Simba.

Mchezo huo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya robo fainali utachezwa Jumamosi ya Aprili 13 nchini Congo. 

Simba mpaka sasa ligi kuu imecheza michezo 22 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia pointi 57. Mpaka sasa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya viporo tofauti na timu mbili zilizo nafasi mbili za juu ambazo ni Azam FC na Yanga.

Azam FC ambayo ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 63 baada ya kucheza michezo 30 huku Yanga ambao ni vinara wana pointi 71 baada ya kucheza michezo 30 na kufanya wabaki na viporo 8 kuwa sawa na wapinzani wao.


4 COMMENTS:

  1. Wapumbavu. Ligi ya kishenz. Unarundka vporo kibao kisa nn? Mbona man city. Barcelona, Tottenham hawana vporo kama simba? Tff wakuda tu

    ReplyDelete
  2. Ligi ya kibabe, viongoz wa tff wakiwa na mapenz na hz timu zetu kubwa kubebana lazma, utawala wa malinzi yanga walikula bata, now zamu ya simba kula batax2 maana kuna mwaka yanga alkuwa na vporo vinne simba akagoma kucheza leo wao wana vporo 8, kweli malipo ni hapa hapa

    ReplyDelete
  3. safi sana tff wacha wanaume wapambanie nchi kinamama wabaki nyumbani wakichambua mchele..........kwani mnateseka?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic