OKWI AZIDI KUWATIA PRESHA SIMBA
Unaambiwa mabosi wa Simba kama vile hivi sasa wanahaha namna ya kumuongezea mkataba straika wao Mganda, Emmanuel Okwi ambao unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa zilizokuja hivi karibuni ni kuwa klabu ya Afrika Kusini, Kaizer Chiefs imeingia katika rada za nyota huyo ili akaanze kuwatumikia moja ya miamba hao wa Afrika Kusini.
Imeelezwa kuwa moja ya vigogo ndani ya Simba amesema kuwa mchezaji huyo ana nafasi ya kuondoka endapo ataamua iwe hivyo na kama akitaka mkataba mpya wala hawana tatizo la kumpa.
Taarifa imesema kuwa mabosi hao wa Simba hawana noma na kuondoka kwa Okwi kwani ni kama mtoto wao kutokana na makubwa aliyoifanyia Simba na hata kama akirudi wanaweza kumpokea tena.
Ikumbukwe Okwi aliwahi kuuzwa kuelekea Etoile Du Sahel ya Tunisia mwaka 2013 na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kuvuna kiasi cha pesa ambacho ni dola 410,000, ukiwa ni usajili wa aina yake uliowahi kufanywa na wekundu hao.
Mara ya mwisho Okwi alivyorejea Simba alisajiliwa na Sports Club Villa ya Uganda kabla ya kutua Simba kisha kusaini miaka miwili ambayo inamalizika baada ya msimu huu.
Simba hawawezi kuhaha kumuongezea mkataba Okwi wakati wana maombi zaidi ya wachezaji mia moja wanaotaka kujiunga na Simba. Simba Kwa sasa inachofocus zaidi ni ushiriki wao wa klabu bingwa Africa na wasingependa kwa wakati huu kuona mchezaji yeyote anawatoa mchezoni kwa sasa. Okwii Simba kwao sawa na Mputu na Mazembe yake. Okwi anaweza kuondoka Simba na kwenda kujaribu bahati sehemu nyengine na akarudi Simba na wala lisiwe shindo nyinyi waabdishi mnaandika vitu kama vile mmekuja leo mjini.
ReplyDelete