UONGOZI wa timu ya Simba umetoa tamko baada ya kulalamikia mabadiliko ya ghafla ya waamuzi wa mchezo wa marudiano kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe, utakaochezwa Mjini Lubumbashi Jumamosi ya Aprili 13.
Shirikisho la soka Afrika CAF limeteua waamuzi wapya ambapo watatu kati yao ni kutoka Zambia wakiongozwa na Janny Sikazwe, Romeo Kasengele na Audrick Nkole.
Waamuzi hao wamechukua nafasi ya waamuzi kutoka Ethiopia na Kenya waliopangwa awali wakiongozwa na Bamlak Tessema Weyesa, Temesgin Samuel Atango.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema CAF ni chombo imara anaamini kitatoa maamuzi ya haki na lengo lao ni kuona anapatikana bingwa halali wa Afrika.
" Tunataka fair play, tunataka haki, tunataka bingwa halali wa Afrika, wao walilalamika Caf why iwe nongwa sisi kulalamika?.
" Ila hawatutoi mchezoni hata tone na wala haitatuondolea concentration (umakini) yetu uwanjani.
" Simba sio klabu ya hovyo hovyo unayoweza kuibabaisha, CAF ni chombo makini na chenye heshma so tunaamini watasikiliza complains (malalamiko) zetu na kuzitolea maamuzi sahihi," amesema Manara.
Manara anastahaki kila aina ya pongezi ni kiongozi anaejuwa nini anachokisema, hana woga na anajiamini anaeipigania timu yake kwa uwezo wake wote na hana husuda za kumtakia yeyote ubaya na asiyekuwa na ubabaishaji wa aina yeyote
ReplyDeleteUoga tuu umewajaa,subirini kugegedwaaa huko maana jamaa wanakula hadi nyani!
DeleteKweli tupu mkuu.
ReplyDelete