April 7, 2019


Kwa kiwango na takwimu za uwanjani walizoonyesha Simba jana dhidi ya TP Mazembe uwezekano upo wa kufuzu nusu fainali.

Katika mechi hiyo ya kwanza ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ilitawala kwenye umiliki wa mpira, pasi na kila kitu kama inavyoonekana kwenye jedwali.

Lakini ukiachana na takwimu hizo, Mazembe waliingiwa hofu na matokeo hayo kutokana na takwimu za msimu uliopita ambapo walitoka suluhu na Agosto nchini Angola lakini wakaenda kutoa sare ya bao 1-1 Lubumbashi na kutolewa.

Katika mechi ya jana, Mohammed Tshabalala wa Simba na Jackson Muleka wa Mazembe ndiyo wachezaji pekee walionyeshwa kadi za njano hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Tshabalala alimchezea vibaya Sissoko wakati Muleka alidanganya kuanguka ndani ya eneo la penalti katika mchezo huo ambao Paschal Wawa alitolewa dakika tatu za kwanza baada ya kuchezewa rafu na nafasi yake kuchukuliwa na Juuko Murshid.

Simba walifanya shambulio moja kali la dakika ya 31 Kagere alipiga mpira wa tiktak iliyogonga mwamba na kurudi kisha akapiga shuti liliokolewa.

Mazembe wao walifanya shambulio moja la Muleka kuudokoa mpira wa juu na kumuacha Wawa kisha kuingia katika eneo la penalti na kujiangusha.

Kipindi cha pili, Simba walimtoa Clatous Chama na kuingia Emmanuel Okwi, Mazembe wao waliwatoa Kalaba na Sissoko na Mputu na kuwaingiza Meshack Elia, Glody Likonza na Nathan Sinkala.

Simba walipata penalti dakika ya 57 Kagere akimshikisha Ochaya, Bocco akapiga na kupaisha.

Bocco alikosa nafasi tatu za wazi katika kipindi cha pili, dakika ya 48 shuti lake liligonga nyavu ndogo, dakika 53 alikosa nafasi akiwa na kipa mpira aliopiga kuokolewa na penalti dakika ya 58.

Simba walipata faulo za nje ya 18 tatu lakini zote hazikuwa na faida.

Mazembe walifanya shambulio moja la hatari la kugongeana pasi za haraka mpira wa mwisho uliopigwa na Likonza uligonga mwamba na kurudi uwanjani mashabiki wa Simba wakavuta pumzi.


Kocha wa Simba, Patrick Aussems alisema; “Nimeridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu ingawa tumekosa nafasi nyingi za wazi, kwenye mchezo wa marudiano Jumamosi tutajirekebisha.”

Lakini Mihayo Kazembe ambaye ni Kocha wa Mazembe alisema wamekosa nafasi nyingi na ni hali ya kawaida kwenye mchezo, watakwenda Lubumbashi kutumia faida ya uwanja wa nyumbani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic