April 7, 2019


Kauli nne nzito alizozingumza Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera kuhusiana na klabu.

"Katika muda niliofanya kazi hapa, nimesoma na kujifunza vitu vingi sana hata kwa hiki nnachoshuhudia leo hakika kimenipa hamasa sana! msimu ujao hatutoumia.

Nimetembea karibu nchi zote za Afrika nikiwa na timu ya Taifa, nawahakikishieni hakuna hata nchi moja yenye mashabiki kama hawa wa Yanga, hata TP Mazembe haina fanbase kubwa kama Yanga. .

Najiuliza kuna ulazima gani timu kama hii eti kungoja tajiri mmoja aje awekeze pesa zake wakati wenyewe mnasema hii ni timu ya wananchi?

"Kwanini wananchi tusiibebe timu yetu wenyewe? Sasa tunapaswa kuibeba wenyewe, timu kama Yanga SC inapaswa kushindania makombe makubwa Afrika. Naomba tuichangie Yanga"

5 COMMENTS:

  1. Kwa hakika Yanga ingekuwa na mhamasishaji au wahamasishaji wenye kujua jinsi gani ya kujenga hamasa kwa mashabiki kuichangia klabu isingekosekana Billion moja kwa kila mwezi lakini huyo msemaji wa klabu yupo pale kuuza sura tu hajui nini cha kufanya,ukienda kwa yule mzee Akilimaji ambae kwa umri wake alipaswa kutumia hekima na busara zake kuwahamasisha mashabiki wa klabu yeye ndo kageuka kuwa kidudu mtu kazi kupita pita maofisini kwa watu kuomba omba hela ya unga huku akisababisha kuchochea migogoro....Yakiwekwa malengo ya kuwafikia mashabiki laki tano kwa michango ya Sh.2,000 hakika Yanga haitayumba

    ReplyDelete
  2. Wamekalia kuiombea Simba mabaya huku kwao kunaungua.

    ReplyDelete
  3. kwa staili hii ya kuchangishana ni kuongopeana.Yanga ilianzishwa 1934 na tokea kipindi hicho imepitia ktk mazingara kama hayohayo ya kuindesha klabu. Nina ufahamu wa kutosha kuhusu klabu hizi mbili za Yanga na Simba tokea miaka ya 1968.Yanga ikiwa chini ya mwenyekiti Kitwana kondo, Mzee Tabu Mangara, Mbwambo, Bocco, Mpondela n.k.pia na wafadhili kina Sharrif Shiraz, Virani,Gulamali,Murtadha Dewji lakini bado hakuna mafanikio.Kwa muono wangu kile Simba wanachokifanya sasa kuna mwanga ktk tunnel.Wamerekebisha katiba, wamebadilisha muundo wa uendashaji wa klabu na haimilikiwi na Dewji pekee yake na hapo ndipo watu wengi wanashindwa kuelewa kuwa Simba inaendeshwa kwa umiliki wa Hisa wa wanachama wanaomiliki 51% na 49% mwekezaji wao Mo Dewji kama klabu nyingi za mpira hapa duniani zinavyoendeshwa.Sasa sioni issue ya kuchangishana kila siku au mwezi itaifikisha timu ktk kujiendesha kisasa.Inabidi wanayanga kabla ya kuchangishana ifanye uchaguzi wa kuzingatia katiba ya klabu na baada ya hapo watakaochaguliwa warudi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kuiendesha klabu ktk misingi itakayokubaliwa na sio hii ya kukutana kwenye mahoteli na kujiamullia kufanya michango.Je hizi pesa za michango zitafanyiwa ukaguzi?zitakuwa kwenye mikono salama?Je kuna uhakika gani wa kukusanya michango kila mwezi kutoka kwa kila mwanachama wakati idadi tu ya wanaolipia kadi zao haizidi hata asilimia 20%?Wakati sie Yanga tunatembea lkn wenzetu wameamua kukimbia na nina uhakika wakiendelea kukaza watapiga hatua.Angalia tu mwitikio wa mashabiki wao wanaojitokeza pale uwanja wa Mkapa au hata mikoani.Angalieni tamasha lao la Simba day la kila mwaka linavyowaingizia pesa.Mie ningewasihii tuangalie fursa zaidi ya hii ya kuchangishana.Ni hoja zangu binafsi hivyo itapendenza kujibiwa kwa hoja za kistaarabu kwani ungwana sio matusi.Nawasilisha.

    ReplyDelete
  4. Umesema kweli tupu. Lakini kinachohuzunisha hakuna atakayetilia maanani mchango wako wa mawazo. Hizo pesa zisipochukuliwa tahadhari zitapigwa na wanjanja.

    ReplyDelete
  5. kaka umenena ukweli lakin mi naona viongozi wengi hata wa juu wanaipiga majungu simba lakin simba imechagua njia sahihi huwezi kuwa club kubwa kwa michango ya matamasha la harambee za mahotelini angalia zahera anachozungumza ni kuwazodoa simba badala ya kuwaelezea ukweli njia sahihi ya kufanya. je tukikusanya bilioni moja, mishahara ya hao wa bilini moja itatoka wapi kama sio kuleta migomo tena?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic