April 21, 2019


BAADA ya jana kunyooshwa mbele ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 2-1 kikosi cha Simba leo kimetua Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance utakaochezwa Aprili 23 Uwanja wa CCM Kirumba.

Simba itashuka kwenye uwanja huo ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja huo kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbao FC hali iliyompa wakati mgumu Mbelgiji Patrick Aussems kwa kutupiwa makopo na mashabiki wa Simba.

Mchezo wa kwanza walicheza na Alliance ambayo imepanda ligi msimu huu uwanja wa Taifa na Simba ilishinda mabao 5-1.

Simba ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 23 ikijikusanyia pointi 60 huku Alliance wakiwa nafasi ya 15 baada ya kucheza michezo 32 wakiwa na pointi 37.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic