April 21, 2019


BAADA ya kikosi cha Mtibwa Sugar kuibuka kidedea mbele ya Yanga kwa ushindi wa bao 1-0 uwanja wa Jamhuri Morogoro kisha Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kulalamikia maamuzi ya waamuzi, uongozi wa Mtibwa Sugar umeibuka na kupinga vikali malalamiko hayo.
Mtibwa Sugar ambayo ipo chini ya kocha mzawa, Zuber Katwila, mchezo wa kwanza dhidi ya Yanga uliochezwa uwanja wa Taifa alipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 na kuziacha pointi tatu Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa anashangazwa na taarifa zinazoelezwa kwamba wamebebwa ilihali mpira ulikuwa wazi na kila mmoja amaeona namna Mtibwa walivyotakata kwenye uwanja wao wa nyumbani.
"Niliwaambia mapema ndugu zangu wa Yanga kwamba hapa ni lazima tuwachape kama ambavyo wao walifanya kwao, hicho ndicho kilichotokea na tumebeba pointi tatu, nashangaa wanadai tumebebwa wakati tuliwazidi mbinu na juhudi uwanjani wapinzani wetu wanapaswa wajipange.
"Kinachowauma Yanga najua wanaona Mtibwa tumewapunguzia kasi na nguvu ya kuendelea kubaki kileleni ila nasi hatukuwa na namna maana tunataka tuwe ndani ya timu tatu bora sasa hatuwezi kufika hapo kama tutafungwa kiwepesi, tunajiamini na tunapambana kwa kila anayefuata hapa ni lazima tumyooshe," amesema Kifaru.
Mtibwa Sugar imecheza michezo 32 imejikusanyia pointi 48 ikiwa nafasi ya nne imeshinda michezo 14, sare 6 na imepoteza michezo 12.

Kutoka Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic