KMC Kesho watakuwa na kibarua kingine mbele ya Singida United uwanja wa Namfua huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao uliopita mbele ya Mbeya City kwa kuchapwa bao 1-0.
Kmc iliyo chini ya Kocha Ettiene Ndiyaragije itacheza mchezo wake na Singida United iliyo chini ya Felix Minziro.
Minziro ametoka kumyoosha Kagera Sugar mabao 2-1 uwanja wa Namfua atamenyana na KMC aliyetoka kupoteza.
Kwa sasa KMC ipo nafasi ya 7 baada ya kucheza michezo 30 ikiwa imekusanya pointi 41 huku Singida United ikiwa nafasi ya 12 baada ya kucheza michezo 32 ina pointi 39.
0 COMMENTS:
Post a Comment