April 30, 2019


KOCHA wa Azam FC, Meja Abdul Mingange amesema kuwa uzoefu umewaponza wachezaji wake hali iliyowafanya wakafungwa bao 1-0 na Yanga kwenye mchezo wao wa ligi uliochezwa jana uwanja wa Uhuru.

Azam FC ilifungwa bao hilo na Mrisho Ngasa ambaye alikuwa mchezaji wao wa zamani dakika ya 13 na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuwafanya wapoteze pointi tatu muhimu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mingange amesema kuwa walijipanga kiasi cha kutosha kupata ushindi kwenye mchezo wao ila walizidiwa uzoefu na wapinzani wao ambao walidhamiria kushinda.

"Haikuwa mipango yetu kupoteza mchezo wetu mbele ya Yanga, tulijipanga kiasi cha kutosha kushinda ila uzoefu wa wachezaji wangu ukatufelisha kwenye mchezo wetu.

"Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wengi ambao wanauzoefu na ligi tofauti na sisi, licha ya kutengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wetu tulishindwa kupata matokeo kutokana na kushindwa kuzitumia nafasi tulizotengeneza," amesema Mingange.

Azam FC wanasalia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 66 baada ya kucheza michezo 33 kwenye ligi kuu huku Yanga wakijikita kileleni na pointi zao 77 kibindoni.

3 COMMENTS:

  1. Sio sababu, wachezaji wazoefu wa TPL pale Yanga ni Chikupe, Ngassa, Gadiel, Shishimbi na Loti, ila Azam wapo kibao wana misimu zaidi ya mmoja.. Abalora, Yakubu, Kingue, Mudathiri, Abu Salum, Ngoma, Chirwa, Lyanga, Agyei, Kangwa hao wote wanaijua TPL, Waseme tu shida ni Uyanga na Usimba ndio unaimaliza Azam hasa Uyanga maana wako wachezaji walicheza Yanga na Sure boy ni mnazi wa Ynaga.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kuropoka nawewe Kwan sure boy ndio aliwashawishi wenzake wafungwe, na mechi ya ndanda je?Kwan azam ni nan asifungwe Kwan huyo sure boy angekaa nje ndio wangeshinda?

      Delete
  2. Hii ndiyo ya mbaazi na jua; kila ukikosa maua ni kusingizia jua!
    Azam keshafungwa na Ndanda, Mwadui na Lipuli, Mingange anataka kusema hawa wote wanaizidi Azam uzoefu?! Kwamba demu aliyeachika ndiye bora zaidi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic