TFF HII NI BALAA ASIKWAMBIE MTU, WATATU AZAM YAWAKUTA
Wachezaji watatu wa timu ya Azam FC wamekutana na rungu la Bodi ya Ligi kwa kusimamishwa michezo mitatu na faini kiasi cha shilingi 500,000.
Faini hiyo imekuja kutokana na kosa la kumzonga Mwamuzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya wenyeji Coastal Union dhidi ya Azam FC huko Tanga
Wachezaji waliokumbwa na rungu hilo ni Ramadhani Singano, Tafazwa Kutinyu na Stephan Kingue Mpondo.
Huu ni uonevu. Kuna timu inapiga marefa licha ya kuzonga lakini hatua hazichukuliwi. Azsm wacheni kuwa wastaarabu mtaburuzwa kwa faida ya timu fulani.
ReplyDelete