April 9, 2019


MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, mbaraka Yusuph, anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi tisa ijayo baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti jijini Cape Town, Afrika Kusini jana.

Nyota huyo amekutwa na tatizo la kuchanika mtulinga wa kati wa goti lake la mguu wa kulia (Anterior Cruciate Ligament Tear), hali iliyolazimika afanyiwe upasuaji huo.

Yusuph aliyepata majeraha hayo wakati akiwa kwenye kikosi cha Namungo kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (FDL), iliyomchukua kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu, amefanyiwa upasuaji huo katika Hospitali ya Vincent Pallotti iliyopo nchini humo.

Daktari wa Azam FC, Dr. Mwanandi Mwankemwa, aliyeongozana na mshambuliaji huyo nchini humo kushughulikia matibabu yake, ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa Yusuph anatarajia kurejea tena uwanjani kwa ajili ya ushindani Desemba 8 mwaka huu. 
#GetWellSoonMbaraka24

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic