WAMBURA AMJIBU ZAHERA KUHUSIANA NA VIPORO VYA SIMBA
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Boniface Wambura, amemweleza Kocha wa Yanga, mwinyi Zahera, kutokuwa na hofu juu ya mechi za viporo ambayo Simba wanakabiliwa navyo.
Kauli ya Wambura imekuja mara baada ya Zahera kulalamika kila wakati kuhusiana na ratiba ya Simba hivyo mpaka imepelekea kuwa na mechi nyingi mkononi ambazo hazijachezwa mpaka sasa.
Wambura amesema kuwa sababu ya mechi nyingi kutochezwa ni kutokana na changamoto ya viwanja pamoja na ugumu wa ratiba.
Bosi huyo wa Bodi ya Ligi amesema hamna timu ambayo imeandaliwa kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania Bara kama wengine wanavyodai mabadiliko ya ratiba ya Simba ni kutokana na ratiba ngumu iliyokuwa nayo kwenye michuano ya kimataifa.
Simba ikirudi kutoka DR Congo italazimika kucheza mechi nyingi ili wasivurunge kalenda ya msimu Pia Wambura amesema leo watatoa ratiba nzima ya Simba na viporo vyake.
Na Mechi za Yanga na Azam pia mmechelewesha ili kuipa ugumu Yanga sababu mnajua wamiliki wa Azam wana mapenzi na Simba ndio mkaamua kuzichelewesha ili Juhudi zifanyike Azam imsimamishe yanga kila pale simba inapotetereka !!! mbona kila kitu kipo wazi kabisa mwenye macho haambiwi tazama na wana yanga tuna akili ya kufikiri msitufanye vilaza !!
ReplyDeleteMbona mlipopangiwa mechi 11 nyumbani na hata kubadilishiwa mechi na Mtibwa ili mcheze nyumbani hamkulalamika?
ReplyDeleteChezeni mpira. KILA MTU ASHINDE MECHI ZAKE.HAKUNA NAMNA.
Kuhusu mechi na Azam mnabebwa nyinyi ili kuwajengea mazingira ya kukaa kileleni.Mechi na Azam imeahirishwa mara mbili kwanini hamkulalamika?
Mmepangwa na vibonde mechi zote mbili ili kuwatengenezea mazingira ya kushinda .
Mliwahi mwaka 2016 kubebwa na kucheza mechi zote mbili na Ndanda nyumbani Dar ili mchukue ubingwa kirahisi .Sasa mbeleko hamna shinda kwa uwezo wako.
Mwanzoni mlikuwa hamlalamiki sasa mambo yameanza kuwa magumu mnatafuta mchawi.
Zahera alikataa ratiba iliyotoka kwanza kabisa eti sababu Simba anaanza mechi tatu za ligi Dar, wac
ReplyDeletekati Yanga anaanza ugenini.Baadaye zikaja figisu za kuwa Yanga haina hela..Akapewa kuanza mechi 11 zote Dar!Ikawa furaha ilioje Jangwani!
Tunajua Athari za jucheza kila baada ya saa 72 yeye mbona Zahera alilalamikia hilo alipoanza kufungwa na Stend United zikafuatia droo mbili mfululizo?.Na tunajua Zahera angependa Simba icheze kila baada ya saa 72 ili wafanye vibaya kwa Wakongo..Sio Simba walioleta mvua Morogoro?Na sio sawa Simba ingecheza mechi katikati ya wiki hii wakati wikiendi wana mchezo wa kufa na kupona Lubumbashi. Zahera aondoe wasiwasi akijua kwamba kwa takwimu sasa hivi hata Simba akita droo mbili na Yanga ashinde mechi zake zote...Ubingwa bado unaenda msimbazi. Kama Yanga alipata unafuu wakati wa mzunguko wa kwanza na sasa ana ugumu, yote alijitakia Yanga, sote tulijua itakuja wagharimu maana mzunguko wa pili hata timi rahisi hukaza zisishuke daraja!
Msimu ujao apewe Zahera aandae ratiba
ReplyDelete