April 7, 2019


ASLAY Isihaka Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ngoma ya 'angekuona' ilimpaisha kimataifa anatarajiwa kushuka Sikukuu ya Pasaka ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.

Meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’ amesema kwa mara ya kwanza tangu Aslay afanye muziki kivyake hajawahi kushuka katika uwanja huo wa taifa wa burudani.

“Siyo Dar Live tu, Aslay hajawahi kufanya shoo yoyote si Temeke wala Mbagala kwa hiyo kwa mara ya kwanza atashuka Dar Live Pasaka hii na kuporomosha vibao vyake kibao kuanzia Hauna, Natamba, Totoa, Nibebe, Likizo na Kwatu hivyo niwaombe mashabiki wote mjitokeze kwa wingi kushuhudia shoo hii ya kihistoria,” amesema KP

Aslay amesema zipo zawadi nyingi amewatayarishia mashabiki wake hivyo wajitokeze kama wote.

“Mashabiki wote mnajua linapokuja suala la shoo huwa silembi, nitakamua live kwa kutumia vyombo hakuna cha ‘playback’ mwanzo mwisho ni burudani tu,” amesema Aslay.

Burudani hiyo ya kijanja itakuwa kwa mchongo wa buku 10 tu yaani 10,000 na 8,000 kwa watu 100 wa kwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic