April 4, 2019


MTWARA, Tanzania - Young Africans imeshindwa kutamba mbele ya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara katika mchezo wa  Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kubanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1.

Yanga waliokuwa wenyeji walianza kufungwa bao la kwanza kupitia mnamo dakika ya 19 kwa Vitalis Mayanga aliyemzidi ujanja beki Kelvin Yondani kisha kumpiga chenga kipa Klaus Kindoki na kupasia mpira nyavuni.

Ilichukua dakika moja pekee kwa bao hilo na katika dakika ya 20 Yanga walipata penati baada ya mshambuliaji wake, Heritier Makambo kuangushwa kunako eneo la hatari na mchezaji wa Ndanda.

Penati hiyo ilishindwa kuzama nyavuni baada ya mpigaji, Mrundi, Amis Tambwe, kupiga mpira ulioenda nje ya lango la Ndanda na kumsaidia kipa wake Said Nduda ambaye alikuwa ameelekea upande tofauti.

Mpaka dakika 45 za kwanza zinamalizika, Ndanda walikuwa kifua mbele kwa bao hilo moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga wakijaribu kufanya jitihada za kutafuta bao la kusawazisha ambazo zilizaa matunda mnamo dakika ya 61 kwa Papy Tshishimbi kuisawazishia kwa njia ya kichwa nkupitia mpira wa krosi uliopigwa kushoto mwa uwanja.

Bao la Tshishimbi lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika kwenye Uwanja huo, matokeo yakiwa ni 1-1.

Katika kipute hicho, Kocha Mwinyi Zahera aliwafanyia mabadiliko baadhi ya wachezaji wake kipindi cha pili kwa kumtoa Tambwe na kumuingiza Deus Kaseke, pia Jaffary Kibaya na kumuingiza Rafae Daudi.

Msimamo wa ligi hivi sasa unaonesha kuwa Yanga bado ipo kileleni ikiwa na alama 68 baada ya kuongeza moja leo huku Ndanda wakifikisha alama 37 kwenye nafasi ya 15.

Imeandaliwa na George Mganga

6 COMMENTS:

  1. Lakini kocha Zahera ana hakika bado ya kuchukuwa ubingwa na Cheche wa Azam anakungojeeni kwa hamu kubwa

    ReplyDelete
  2. Yanga mtulie mtathmini namna mtakavyoweza kufanya yafuatayo kwa ajili ya kufikia malengo yenu ya kuchukua ubingwa

    1. Kuinua kiwango cha uchezaji wa timu kwa ujumla.

    2. Mbinu na staili za ufundishaji baadhi ya waalimu katika benchi la ufundi uwezo wao ni mdogo sana....mfano kocha wa viungo na utimamu wa mwili, Noel Mwandila na kocha wa makipa Juma Pondamali.

    3. Idara ya matibabu na wachua misuli sijui ni kwanini wachezaji wanaumia na kuchukua muda mrefu kupona.

    4. Nidhamu ya mchezo kwa wachezaji makosa madogo madogo yanayojirudiarudia!.

    5. Hamasa na fedha za wachezaji ili kutoa motisha ya ushindi....

    6. Kutafuta mbinu bora as namna ya kukabiliana na maadui ndani na nje ya uwanja kabla na wakati wa mechi na mashindano!

    Kama kuna mwanayanga anasoma huu UJUMBE autume kwa wanaohusika!...

    ReplyDelete
  3. Naona kimahesabu kuchukua ubingwa kwa Yanga zimeshakataa na asipokaza hata FA cup atalisikia kwenye bomba

    ReplyDelete
  4. Wacha wakomae nä visivyowahuhusu.Watakosa vyote.

    ReplyDelete
  5. Naendelea kujiuliza kocha Zahera anapoendelea kusema Yanga watachukua ubingwa !! itawezekanaje? Mi naona anatupiga siasa tu.

    ReplyDelete
  6. Hata Mnyika kasema leo kuwa Yanga ina nafasi.Inawezekanaa endapo atamfunga Azam mechi zote mbili na amuombee simba kupoteza na sare

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic