April 8, 2019


NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa sare waliyoipata mbele ya Ndanda imewapa maumivu hivyo leo watapambana mbele ya African Lyon kupata pointi tatu.

Yanga itacheza leo na African Lyon mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba huku wakiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo wao uliopita kwa bao 1-0 uliochezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

"Tumejipanga kwa ajili ya kupambana na kupata ushindi mbele ya Lyon, tunawaheshimu wapinzani wetu wapo imara na bora ndio maana wanashiriki ligi ila kikubwa ambacho tunahitaji ni pointi tatu, mashabiki watupe sapoti," amesema Abdul.

Lyon ipo nafasi ya 20 baada ya kucheza michezo 32 ikiwa imejikusanyia pointi 22 huku Yanga ikiwa nafasi ya kwanza na ina pointi 68 baada ya kucheza michezo 29.

1 COMMENTS:

  1. Orodha iliyotoka katika kuchukua fomu za kugombea uongozi katika uchaguzi wa Yanga inaonekana kuna watu/waliochukua fomu baadhi yao hata uhalali wa uanachama/upenzi wao katika klabu ya Yanga una ulakini.... walakini....mfano sijui kama Dk Mshindo Msola na Fredrerick Mwakalebela ni Yanga. Pia kuna waliochukua fomu ambao walishashindwa kuongoza taasisi mbalimbali za serikali au michezo huko nyuma na kukumbwa na kashfa mbalimbali zikiwemo Ubadhirifu wa pesa, kutoa ama kupokea rushwa lakini nao pia wamejitokeza....wanachama wa Yanga wanatakiwa kuwa makini mno....kuchuja mamluki na wale ambao hawana maslahi na klabu na maendeleo ya mpira wa miguu nchini....Viongozi wanaotakiwa ni wale ambao ni waadilifu na walio na vision na ubunifu katika katika kuitoa klabu hapo ilipo na kuipeleka katika level ya juu ya maendeleo kulingana na ukubwa wa klabu ulivyo....na kuifanya ijitegemee...wanachama lazima watambue walipotoka wapi walipo na wapi wanataka kwenda....historia yao ya uanachama wa Yanga, historia ya mgombea mmoja mmoja lazima iainishwe na iwekwe wazi ushiriki wake huko nyuma katika kuisaidia klabu kimawazo, fedha na hali yoyote ile...ili wapimwe uwezo wao kabla ya kupewa madaraka!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic