April 8, 2019



RUVU Shooting ya Masau Bwire, jana ilikubali kupoteza mbele ya Stand United mchezo uliochezwa Uwanja wa Kambarage kwa kufungwa bao 1-0.

Bao pekee lililofungwa dakika ya 70 na Majid Kibondile lilitosha kuwapa pointi tatu muhimu Stand United.

Matokeo hayo yanaifanya Stand United kupanda kwa nafasi nne ikitoka nafasi ya 17 mpaka nafasi ya 13 kwa sasa baada ya kucheza michezo 33 ikiwa na pointi 39.

Ruvu Shooting inashuka kutoka nafasi ya 16 mpaka ya 18 ikiwa imecheza michezo 33 imejikusanyia pointi 36.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic