April 2, 2019

TIMU ya Simba imetangaza viingilio katika mchezo wao wa r obo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe utakachezwa Jumamosi Aprili 6, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara, amesema kiingilio cha chini kitakuwa ni shilingi 4,000 (Mzunguko) kwa watakaonunua tiketi mapema kuanzia leo Aprili 2, hadi Ijumaa saa 6:00 usiku lakini siku ya Jumamosi tiketi hizo zitapatikana kwa shilingi 5,000.

Viingilio vingine ni shilingi 10,000 kwa VIP A, shilingi 20,000 kwa VIP B, na shilingi 100,000 kwa tiketi za Platinum.




Manara amesema kauli mbiu itakayotumika kwenye mchezo huo ni ‘YES WE CAN” kwa mara nyingin tena.


 “Tunakwenda na Slogan ileile ya Yes We Can, kwakuwa imelipa na inatuweka salama zaidi huku tukicheza bila presha!! Tutawakabili Mazembe huku tukiujua ubora wao lakini Simba ishazoea kuishangaza Afrika na dunia kwa ujumla na tutafanya hivyo Jumamosi," amesema Manara.


Kwa mara ya kwanza Yes We Can ilitumika katika mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya JS Saoura uliochezwa Uwanja wa Taifa na Simba ilishinda mabao 3-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic