LICHA ya kushindwa kutambajana mbele ya Mbao FC wakiwa uwanja wa nyumbani kwa kugawana pointi moja, Mwadui FC wamesema kuwa bado wana nafasi ya kusalia Ligi Kuu Bara, msimu ujao.
Kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Complex walilazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 hali iliyofanya wasalie nafasi ya 19 wakiwa na pointi 38.
Akizungumza na Saleh Jembe, kinara wa kupachika mabao kwa sasa kwenye kikosi hicho, Salim Aiyee amesema kuwa wana imani ya kujikusanyia pointi tatu kwenye michezo yao miwili iliyobaki.
"Bado tunapambana kuona ni namna gani tutapata matokeo, ushindani ni mkubwa na kila timu inatafuta ushindi hivyo tutapambana kwenye mechi zetu mbili ambazo zimebaki," amesema Aiyee mwenye mabao 16.
Mechi mbili ambazo wamebakiwa nazo kwa sasa mkononi Mwadui ni pamoja na ule dhidi ya African Lyon pamoja na Ndanda FC yote watacheza uwanja wa Mwadui Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment