May 14, 2019


IMEELEZWA kwamba kutokana na kikosi cha Yanga, kuachana rasmi na aliyekuwa mlinda mlango namba moja wa kikosi hicho Beno Kakolanya wameanza kuiwinda saini ya mlinda mlango namba wa timu ya Taifa anayetumikia Mbao, Metecha Mnata.

Yanga kwa sasa imekuwa na tatizo kwenye upande wa mlinda mlango kutokana na Klaus Kindoki ambaye ni raia wa Congo kuwa na makosa mengi ya kiufundi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Metacha Mnata amesema kuwa kwa sasa bado hajapata taaarifa hizo anachotambua yeye anaitumikia Mbao, hivyo kama watakuwa wanahitaji saini yake utaratibu upo wazi.

"Mimi napambana na timu yangu ambayo naitumikia kwa sasa, nayo ni Mbao kama kuna habari nyingine bado sijapata taarifa nina amini utaratibu upo na kila kitu kuhusu mchezaji kinajulikana," amesema kwa kifupi Mnata.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic