May 14, 2019


BAADA ya jana kushindwa kulipa kisasi mbele ya Simba, wachezaji wa Azam FC wamepewa mapumziko ya siku mbili kabla ya kuanza mazoezi kwa ajili ya kuiwinda Mtibwa Sugar.

Azam FC iligawana pointi moja na Simba uwanja wa Uhuru na kushindwa kulipa kisasi cha mabao 3-1 waliyofungwa uwanja wa Taifa mzunguko wa kwanza wa ligi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa wanatambua watakuwa wana kazi nyingine ngumu mbele ila kwa sasa wamewapa mapumziko wachezaji wao.

"Tumewapa mapumziko wachezaji wetu ya siku mbili kabla ya kuanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata.

"Leo na kesho wachezaji watapumzika ili kujiweka sawa, ila baada ya hapo tutaanza mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu unaofuata," amesema Alando.

Mchezo wa Azam FC unaofuata Ligi Kuu Bara utakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa uwanja wa Chamazi, Mei 22.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic