May 14, 2019


KIUNGO mshambuliaji wa timu ya Simba, Hassan Dilunga amesema kuwa watatumia mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Sevilla ambao umeandaliwa na kampuni ya kubashiri Tanzania SpotPesa kujitangaza kimataifa.

Simba ambao ni washindi wa tatu kwenye michuano ya SportPesa Cup iliyofanyika uwanja wa Taifa Dar, itamenyana na Sevilla, Mei 23 huku mabingwa hao mara tano wa UEFA wakitarajiwa kutua nchini Mei 21.

"Ni jambo la furaha kwetu kupata nafasi ya kucheza na kikosi cha Sevilla, nina imani utakuwa ni mchezo mzuri na wenye kuvutia kutokana na aina ya wachezaji ambao tutacheza nao, hivyo tutatumia mchezo huo kuwa sehemu ya kujitangaza.

"Kila mchezaji ana morali na ari ya kupambana  na imani yetu kufanya vizuri na itatufanya tuzidi kujiamini zaidi katika michezo yetu mingine," amesema Dilunga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic