May 24, 2019


Jose Mourinho amesema kuwa anaona anguko lingine kwa meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp ambaye ametinga hatua ya fainali mara tatu za Ligi ya Mabingwa Ulaya na zote hajabeba kombe.
Mourinho ambaye alikuwa meneja wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na Manchester United, alishinda mataji yote ya Ligi ya Mabingwa Ulaya alipotinga hatua ya fainali amesema kuwa hana imani na Klopp licha ya kubeba matumaini makubwa kwamba anashida fainali ya msimu huu. 
"Kupoteza kwakwe  akiwa meneja wa Borussia Dortmund mwaka 2013 uwanja wa Wembley kipindi ambacho alikuwa meneja na alipambana tena fainali yake ya pili akiwa na Liverpool uwanja wa Kiev aliambulia kichapo kutoka kwa Real Madrid msimu uliopita.
"Kama  Jurgen (Klopp) atashindwa inakuwa ni ngumu kwangu kuamini na ninaona ni kitu kigumu kutokea kwake, kama atashindwa kushinda atakuwa kwenye wakati mgumu kwani inaumiza kushindwa kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya ilihali umeshiriki fainali mara nyingi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic