May 24, 2019


MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Roberto Firmino amerejea na kuanza mazoezi baada ya kutengamaa afya yake kutokana na kusumbuliwa na majeruhi hivyo ana nafasi ya kuwepo kwenye kikosi kitakachocheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Spurs.
Nyota huyo aliikosa michezo mitatu ambayo Liverpool ilicheza kutokana na kuwa majeruhi lakini amerejea na kujiunga kambini na wachezaji wenzake kwenye kambi ya Marbella
Ikiwa imebaki wiki moja kabla ya Juni mosi ambapo watacheza na Tottenham, meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa mchezaji wake yupo.
"Sio muda mrefu ambao umepita ila ilikuwa ni lazima iwe hivyo kwa ajili ya umakini na kuhakikisha kwamba tunakuwa na matumaini ya yeye kurejea uwanjani na hicho ndicho ambacho kimetokea.
"Tuna siku chache ambazo zimebaki kwetu ndio maana tumekuwa naye katika mazoezi yetu, licha ya kutokuwa pamoja nasi alikuwa anacheza mechi ambazo hazikuwa na mashindano makubwa, hii itamasaidia kuwa kwenye ubora wake," amesema Klopp ambaye anaamini atamtumia Firminho kwenye fainali yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic