May 12, 2019


SIMBA wamejiridhisha kwamba Patrick Aussems ni bonge la kocha na watampa mkataba wa sapraizi punde.

Awali kulikuwa na mvutano ndani ya klabu hiyo juu ya kocha huyo kuendelea ama kutoendelea kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kutokana na madai ya kushindwa kufanya vyema katika mechi za kimataifa timu inapokuwa ugenini.

Akizungumza na Spoti Xtra, Katibu Mkuu wa Simba, Anord Kashembe amefunguka kuwa, Aussems ana asilimia kubwa ya kubaki ndani ya kikosi hicho na kudai kuwa kinachosubiriwa sasa ni ligi ifikie tamati ili wamuekee mzigo mezani.

“Aussems ni kocha mzuri hivyo si rahisi kuachana nae, uongozi unasubiria ligi iishe ili uweze kukutana naye kwa ajili ya kufanya nae mazungumzo ya kuweza kuongeza mkataba mpya.

“Tunachohitaji ni kuhakikisha tunafanikiwa kufanya vizuri msimu ujao kwenye ligi na mechi za kimataifa hivyo kubadili makocha haitakuwa sahihi,” alisema Kashembe.

Kocha huyo ameifikisha Simba kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa lakini baadhi wakawa wanahoji uwezo wake katika mechi za ugenini kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic